Skip to main content

Posts

Mwanajeshi Aliyejeruhiwa na Bomu Sehemu za Siri Apandikizwa Uume

Timu ya madaktari wa nchini Marekani wamefanikiwa kwa mara ya kwanza kwenye historia kufanya upasuaji wa kupandikiza ‘uume’ kwa mwanajeshi aliyejeruhiwa vibaya sehemu za siri. Inaelezwa kuwa mwanajeshi huyo alijeruhiwa na bomu nchini Afghanistan. Madaktari walifanikiwa kumpandikiza uume pamoja na mfumo wa uzazi mwingine baada ya kupata viungo hivyo kutoka kwa mfadhili wa viungo aliyefariki. Madaktari hao wa upasuaji wa Chuo Kikuu cha Johns Hopkins Baltimore, Maryland wameeleza kuwa kutokana na mafanikio ya upasuaji huo mwanaume huyo atapona kabisa na viungo vyake vitaendelea kufanya kazi kama kawaida.

Kikosi cha Real Madrid Chawasili Mjini Munich

Kikosi cha Real Madrid tayari kipo jijini Munich, Ujerumani tayari kuwavaa wenyeji wao Bayern Munich. Wanakutana katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Madrid wakianzia ugenini. Nyota wao, Cristiano Ronaldo yuko tayari kwa ajili ya mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu. Hata hivyo, tayari Madrid imeonywa kwamba Bayern Munich si timu ya kudharau na wanapaswa kuwa makini sana hiyo kesho.

Ndege Kubwa Zaidi ya Emirates Iliyobeba Abiria 475 Yatua kwa Dharura Dar...

Ndege ya kampuni ya Emirates iliyokuwa ikielekea Mauritius ikiwa na abiria 475 wakitokea Dubai, imetua jijini Dar es Salaam leo kwa dharura kutokana na hali mbaya ya hewa nchini humo.  Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege Tanzania, Kamishna msaidizi, Matanga Mbushi ameithibitishia MCL Digital, taarifa hizo akisema ndege hiyo ya Emirates, aina ya Airbus 380, EK701, ilishindwa kutua mara tatu nchini Mauritius kutokana na mvua kali iliyokuwa ikinyesha.  “Hiyo ndege ilikuwa ikielekea Mauritius, sasa hali ya hewa imekuwa mbaya ikashindwa kutua. Rubani alijaribu kutua mara tatu lakini akashindwa ndipo akaamua kuja Dar es Salaam kutua kwa dharura,” alisema Mbushi.  Amesema ndege hiyo ilikuwa na abiria 475 na wote wamepangiwa hoteli ili kusubiri taarifa za hali ya hewa ikiwa nzuri waendelee na safari.  “Kesho kama hali itakuwa nzuri wataondoka,” amesema Mbushi.  Ndege hiyo ni ya Shirika la Emirates la Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (U...

UK yawatahadharisha Watanzania Kuhusu Maandamano Ya Tarehe 26/04/2018

                London, Uingereza. Serikali ya Uingereza imewataka wananchi wake wanaoishi hapa nchini kuchukua tahadhari na maandamano ya kisiasa yanayotarajiwa kufanyika Aprili 26. Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo Aprili 24 imesema kwamba kuna raia zaidi ya 75,000 wanaoingia nchini hapa kila mwaka. Hivyo imewatahadharisha kujihusisha na maandamano hayo kwa madai kwamba wanaweza kupata madhara kutoka kwa jeshi la polisi. Katika taarifa hiyo ilitolewa tahadhari kwamba kwa sababu maandamano hayo yalishapigwa marufuku hivyo polisi ni lazima watatumia mabomu ya machozi au silaha za moto. “Hivyo muwe makini sana mnapokuwa kwenye mizunguko yenu muepuke mikusanyiko ya watu au watu wanaoandamana, muda wote muwe mnasikiliza vyombo vya habari, mjue nini kinachoendelea,’’ ilisema taarifa hiyo na kuongeza: “Ikiwa mnahitaji mawasiliano na namba ya dharura ya kupiga haraka ni 112 uliza huduma ya d...

Wasanii wachangia Shilingi Laki Tano Msiba wa Jebby

Msanii wa Bongo Fleva, Jebby amezikwa katika makaburi ya Mailimbili mjini Dodoma.  Jebby ambaye amewahi kufanya vizuri na wimbo wake wa ‘Swahiba’ alifariki dunia hapo jana April 22, 2018 mji  ni Dodoma alipokuwa akipatiwa matibabu.  Wapili kushoto ni msanii Suma G.  Kwa mujibu wa mdogo Jebby, Hamis Omary msanii huyo hakubahatika kuwa na mke wala mtoto, pia kuna nyimbo zaidi ya nne alirekodi ambazo zipo tayari ila hazijatoka.  Professor Jay ni miongoni mwa wasanii waliohudhuria katika msiba huo ambapo amekabidhi Tsh. 550,000 zilizochangwa na wasanii kwa ajili ya msiba huo, msanii mwingine aliyehudhuria ni pamoja na Suma G.

Msanii Chegge afunguka hatakuja kumsahau Masogange

MKALI wa Ngoma ya Kaitaba, Said Juma ‘Chegge Chigunda’ amesema miongoni mwa vitu ambavyo hatakuja kuvisahau maishani mwake ni pamoja na msiba wa video vixen, Agnes Gerald ‘Masogange’ uliotokea Ijumaa iliopita. Chege aliyasema hayo juzi Jumapili alipokuwa Viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar katika kuuaga mwili wa Masogange aliyefariki ghafla baada ya kupungukiwa damu. “Kiukweli msiba umeniumiza kama msanii kwani sisi ni miongoni mwa wasanii wa Bongo Fleva wa mwanzomwanzo kumtoa Masogange kimuziki, kifupi sitamsahau na nawapa pole ndugu na wanafamilia,” alisema Chegge. Masogange alitarajiwa kuzikwa nyumbani kwao, Mbalizi-Mbeya jana. Atakumbukwa kwa mchango wake katika tasnia ya muziki wa Bongo Fleva akiwa kama video vixen, kati ya video zake zilizokubalika ni pamoja na Msambinungwa ya Tunda Man pamoja na Masogange ya Belle9.

Pogba: Swala la uhamisho halipo akilini

Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba amesisitiza kuwa mawazo yake yote yapo Manchester United kwa sasa na siyo uhamisho kama wengi wanavyotarajia. Meneja wa Manchester City, Pep Guardiola amewahi kusikika wakati wa derby yake na United akisema kuwa amewahi pata nafasi ya kuzungumza na wakala wa Pogba, Mino Raiola juu ya kumpatia ofa ya kiungo huyo kupitia dirisha la usajili la mwezi Januari. Pogba amerejea kwenye fomu yake wiki za hivi karibuni baada ya kuishindia United ikitoka nyuma na kuibuka na ushindi wa mabao 3 – 2 dhidi ya City  Aprili 7. Kiungo huyo wa timu ya taifa ya Ufaransa amekiambia chombo cha habari cha  Canal Football Club, “Kwa sasa nipo Manchester United na ukweli ni kwamba nafikiria hapa nilipo kwa sasa, swala la uhamisho halipo kichwani mwangu. Tupo fainali yaya FA na kombe la dunia lipo karibu,”amesema Pogba. Hata hivyo Poga amefanikiwa kuibuka nyota wa mchezo wakati wa nusu fainali  ya  FA dhidi ya  Tottenham k...