Skip to main content

Pogba: Swala la uhamisho halipo akilini




Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba amesisitiza kuwa mawazo yake yote yapo Manchester United kwa sasa na siyo uhamisho kama wengi wanavyotarajia.

Meneja wa Manchester City, Pep Guardiola amewahi kusikika wakati wa derby yake na United akisema kuwa amewahi pata nafasi ya kuzungumza na wakala wa Pogba, Mino Raiola juu ya kumpatia ofa ya kiungo huyo kupitia dirisha la usajili la mwezi Januari.

Pogba amerejea kwenye fomu yake wiki za hivi karibuni baada ya kuishindia United ikitoka nyuma na kuibuka na ushindi wa mabao 3 – 2 dhidi ya City  Aprili 7.

Kiungo huyo wa timu ya taifa ya Ufaransa amekiambia chombo cha habari cha  Canal Football Club, “Kwa sasa nipo Manchester United na ukweli ni kwamba nafikiria hapa nilipo kwa sasa, swala la uhamisho halipo kichwani mwangu. Tupo fainali yaya FA na kombe la dunia lipo karibu,”amesema Pogba.

Hata hivyo Poga amefanikiwa kuibuka nyota wa mchezo wakati wa nusu fainali  ya  FA dhidi ya  Tottenham kwa ushindi wa mabao 2 – 1 siku ya Jumamosi.

Comments

Popular posts from this blog

Historia ya mkoa wa kigoma

 Mkoa wa Kigoma  uko kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye postikodi namba 47000. Umepakana na Burundi na Mkoa wa Kagera upande wa Kaskazini, mikoa ya Shinyanga na Tabora upande wa mashariki na Mkoa wa Rukwa upande wa kusini. Magharibi umepakana na Ziwa Tanganyika penye mpaka na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Viwianishi: 4°53′S 29°40′E / 4.883°S 29.667°E Nchi Tanzania Wilaya 8 Mji mkuu Kigoma Serikali - Mkuu wa Mkoa Emmanuel Maganga Eneo - Mkoa 46,066 km² - Bara 37,037 km² - Maji 8,029 km² Idadi ya wakazi (2012) - 2,127,930 Jiografia Mkoa una eneo la km² 45,066 (sawa na 4.8% ya eneo lote la Tanzania) ikiwa km² 8,029 ndizo maji ya ndani (hasa Ziwa Tanganyika) na km² 37,037 ndizo nchi kavu. Takriban robo ya eneo la mkoa wa Kigoma hutumika kwa kilimo na ufugaji, karibu nusu ni misitu. Kwa ujumla eneo la mkoa ni tambarare ya juu inayoanza kwenye mita 800 juu ya UB karibu na Ziwa Tanganyika na kupanda hadi mita 1,750. Mito ya kudumu ndani ya mkoa wa K...

Stendi ya mabasi ya mikoani Ubungo kuhamishwa kupisha kituo cha mabasi ya Mwendo Kasi

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ipo kwenye majadiliano ya kuhamisha kituo cha Mabasi Yaendayo Haraka (UDART), kilichopo Jangwani na kukipeleka kwenye kituo cha Mabasi yaendayo Mikoani Ubungo (UBT). Hatua hiyo inatokana na eneo hilo la Jangwani kukumbwa na mafuriko ya mara kwa mara hali inayosababisha kuharibika kwa magari hayo. Akizungumza kwenye kikao cha kawaida cha madiwani jana, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita, alisema uamuzi huo umefikiwa ili kunusuru magari hayo yasiendelee kuharibika. Alisema Menejimenti ya Kampuni ya UDART na viongozi wa jiji wapo kwenye majadiliano kuhusu suala hilo ili waweze kufikia mwafaka. “Kwa sasa tupo kwenye majadiliano kwa ajili ya kuhamisha kituo cha mabasi yaendayo kasi(UDART) cha Jangwani tuweze kukipeleka Ubungo kwa sababu eneo la Jangwani limekuwa likikumbwa na mafuriko ya mara kwa mara mvua inaponyesha,” alisema Mwita. Alisema suala hilo linaendelea kufanyiwa kazi na Halmashauri ya Jiji hilo ipo kwenye mchakato wa kupanua Mt...

Mabasi ya Mwendokasi yasitisha huduma zake kwa muda

Kampuni inayotoa huduma katika mradi wa mabasi yaendayo haraka (UDART) imeamua kusitisha usafirishaji wa abiria kwa baadhi ya njia kuanzia saa 6:00 mchana kutokana na kufungwa kwa barabara ya Morogoro eneo la Jangwani kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha.  Hayo yameelezwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano UDART, Deus Bugaywa na kusema wamechukua maamuzi hayo kutokana na maji mengi ya mvua kupita juu ya daraja la Mto Msimbazi Jijini Dar es Salaam hali ambayo inahatarisha usalama wa abiria pamoja na vyombo vya usafirishaji.  "Kwa sasa huduma zinatolewa kwa njia za Mbezi - Kimara, Kimara - Morroco, Kimara - Magomeni Mapipa, Kivukoni - Muhimbili, Gerezani - Kvukoni, na Gerezani - Muhimbili. Huduma kamili zitarejea mara baada ya barabara kufunguliwa", amesema Bugaywa. Kwa upande mwingine, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano UDART, Deus Bugaywa amewaomba radhi wananchi wanaotumia usafiri huo kwa usumbufu ambao utajitokeza kwa namna moja ama ny...