Skip to main content

Chris Mauki amtaka Waziri awachukulie hatua Nandy na Bill Nas

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na mshauri wa masuala mbalimbali ya mahusiano Dr. Chris Mauki amefunguka na kutoa maoni yake kuhusu sakata la wasanii Nandy pamoja na Bill Nas kufuatia kuvuja kwa video yao wakiwa faragha.

Mauki ameitaka Wizara inayohusika na masuala ya sanaa ichukue hatua dhidi ya wasanii hao ili kudumisha maadili na nidhamu katika jamii hususani kwa wasanii ambao ni kioo cha jamii na kusewa endapo watafanya hivyo basi litakuwa funzo kwa wasanii wengine na watu wengine katika jamii.

"Mheshimiwa waziri Mwakyembe, Naibu Waziri pamoja na baraza la sanaa chini ya ndugu Mwingereza.

Tutaiona nia yenu ya dhati kabisa kwenye kudumisha maadili na nidhamu katika jamii na hususani kwa wasanii ambao wanajiita "kioo cha jamii" pale ambapo hamtoinyamazia hii hali ya kuanikwa mitandaoni matukio ambayo kiuhalisia yalihitaji privacy, ninasimama sehemu ya ndugu zao hao wahusika, sehemu ya wazazi wao, sehemu ya wadogo zao, na wengine wengi ambao waliwaona kama role models wao.

Kulikoni majukwaani tuwaone kama vioo vya jamii na huku nyuma mitandaoni mnaiharibu kabisa ile picha mliyoichora machoni pa watanzania" Aidha Mauki aliendelea kusisitiza kuwa "Kama ilivyoenea katika public basi tujulishwe katika public ni hatua gani za kinidhamu zinafuata na onyo kwa wengine wenye fikra finyu na chafu kama hawa wanaohalalisha tabia za kingono mitandaoni.

Masikio ya wenye akili na hekima yanasubiri kusikia kutoka kwenu viongozi wetu wenye mpini" alisisitiza Chris Mauki

Comments

Popular posts from this blog

Historia ya mkoa wa kigoma

 Mkoa wa Kigoma  uko kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye postikodi namba 47000. Umepakana na Burundi na Mkoa wa Kagera upande wa Kaskazini, mikoa ya Shinyanga na Tabora upande wa mashariki na Mkoa wa Rukwa upande wa kusini. Magharibi umepakana na Ziwa Tanganyika penye mpaka na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Viwianishi: 4°53′S 29°40′E / 4.883°S 29.667°E Nchi Tanzania Wilaya 8 Mji mkuu Kigoma Serikali - Mkuu wa Mkoa Emmanuel Maganga Eneo - Mkoa 46,066 km² - Bara 37,037 km² - Maji 8,029 km² Idadi ya wakazi (2012) - 2,127,930 Jiografia Mkoa una eneo la km² 45,066 (sawa na 4.8% ya eneo lote la Tanzania) ikiwa km² 8,029 ndizo maji ya ndani (hasa Ziwa Tanganyika) na km² 37,037 ndizo nchi kavu. Takriban robo ya eneo la mkoa wa Kigoma hutumika kwa kilimo na ufugaji, karibu nusu ni misitu. Kwa ujumla eneo la mkoa ni tambarare ya juu inayoanza kwenye mita 800 juu ya UB karibu na Ziwa Tanganyika na kupanda hadi mita 1,750. Mito ya kudumu ndani ya mkoa wa K...

UK yawatahadharisha Watanzania Kuhusu Maandamano Ya Tarehe 26/04/2018

                London, Uingereza. Serikali ya Uingereza imewataka wananchi wake wanaoishi hapa nchini kuchukua tahadhari na maandamano ya kisiasa yanayotarajiwa kufanyika Aprili 26. Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo Aprili 24 imesema kwamba kuna raia zaidi ya 75,000 wanaoingia nchini hapa kila mwaka. Hivyo imewatahadharisha kujihusisha na maandamano hayo kwa madai kwamba wanaweza kupata madhara kutoka kwa jeshi la polisi. Katika taarifa hiyo ilitolewa tahadhari kwamba kwa sababu maandamano hayo yalishapigwa marufuku hivyo polisi ni lazima watatumia mabomu ya machozi au silaha za moto. “Hivyo muwe makini sana mnapokuwa kwenye mizunguko yenu muepuke mikusanyiko ya watu au watu wanaoandamana, muda wote muwe mnasikiliza vyombo vya habari, mjue nini kinachoendelea,’’ ilisema taarifa hiyo na kuongeza: “Ikiwa mnahitaji mawasiliano na namba ya dharura ya kupiga haraka ni 112 uliza huduma ya d...

Diamond Amtumia Salamu Ali Kiba Baada ya Kusikia Amefunga Ndoa

From Daimond "Ni Mwendo wa Picha za Suti tu sasa hivi, Maana nisije nikafungua hata kashati nikajikuta Centro...Pole yenu Wa zee wa Gym, Kama Muscat Round hii🤣🤣🤣.... Wadau Nimeambiwa King Kiba kaoa leo...Mfikishieni Salam zangu, za Ndoa njema, na Maisha yenye Furaha, Amani na Baraka tele...🔥🔥🔥 # SanaaImezaliwaUpya "