Skip to main content

Kanuni Mpya Kudhibiti Matusi na Picha za Uchi Mitandaoni





Serikali imesema kanuni mpya za maudhui kwenye mitandao, runinga na redio zimetungwa kwa lengo la kudhibiti usambazaji wa kauli chafu, matusi, picha za utupu na zenye maudhui yasiyofaa kwa watoto.

Kanuni hizo zimetungwa ikiwa ni utekelezaji wa Sheria ya Mawasiliano ya Kiektroniki na Posta ya Mwaka 2010.

Pia imesema itaendelea kuhamasisha utengenezaji na uzalishaji wa maudhui ya ndani yanayozingatia maadili, mila na desturi za Mtanzania huku ikikiri kuwapo kwa mmomonyoko wa maadili kunakoongezeka siku hadi siku, hivyo imejipanga kukabiliana na changamoto hiyo.

Akiwasilisha bungeni mjini hapa jana hotuba ya makadirio ya bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Waziri wa wizara hiyo, Dk. Harrison Mwakyembe, alisema kanuni hizo zinamtaka kila mtumiaji wa mitandao awe na namba ya siri ili 'wajanja' wasitumie kirahisi chombo chake cha mawasiliano kutenda matendo yanayokwenda kinyume cha sheria.

Alisema kanuni hizo pia zinaweka muda maalumu kwa picha mgando na nyongevu za filamu au muziki wenye maneno yasiyofaa kwa watoto kuonyeshwa kwenye runinga.

"Tuliweka muda huo maalumu kuanzia saa 4:00 usiku hadi saa 11:30 asubuhi, lakini wadau wamekuwa wakali, wanadai picha na nyimbo hizo zirushwe kuanzia saa 6:00 usiku wakati watoto wamelala na mwisho saa 11:00 asubuhi, kabla watoto hawajaamka," alisema Dk. Mwakyembe.

Aliongeza kuwa kanuni hizo zinataka madaraja yawekwe kwa kila filamu, video, wimbo au albamu kutoka ndani au nje ya nchi ndipo kazi hizo zitumike kwenye vyombo vya utangazaji.

"Msingi wa kanuni hizi ni kuhakikisha teknolojia inatutumikia badala ya kututumikisha na kuvuruga mustakabali wa maadili ya taifa letu. Ni kanuni zilizozingatia mazingira yetu halisi kama kila Watanzania," alisema.

Dk. Mwakyembe alisema, mmomonyoko wa maadili ya Kitanzania unaoongezeka siku hadi siku, ni miongoni mwa changamoto zinazoikabili wizara yake.

Alisema wanaendelea kutoa elimu kupitia vyombo vya habari na kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kuzingatia maadili, mila na desturi za Kitanzania.

Ili kutekeleza majukumu yake kwa mwaka ujao wa fedha, Dk. Mwakyembe aliliomba Bunge kuidhinisha bajeti ya Sh. bilioni 33.3. Kati yake, Sh. bilioni 12.2 ni mishahara, Sh. bilioni 9.3 kwa ajili ya matumizi mengine na Sh. bilioni 8.7 za utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Comments

Popular posts from this blog

Historia ya mkoa wa kigoma

 Mkoa wa Kigoma  uko kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye postikodi namba 47000. Umepakana na Burundi na Mkoa wa Kagera upande wa Kaskazini, mikoa ya Shinyanga na Tabora upande wa mashariki na Mkoa wa Rukwa upande wa kusini. Magharibi umepakana na Ziwa Tanganyika penye mpaka na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Viwianishi: 4°53′S 29°40′E / 4.883°S 29.667°E Nchi Tanzania Wilaya 8 Mji mkuu Kigoma Serikali - Mkuu wa Mkoa Emmanuel Maganga Eneo - Mkoa 46,066 km² - Bara 37,037 km² - Maji 8,029 km² Idadi ya wakazi (2012) - 2,127,930 Jiografia Mkoa una eneo la km² 45,066 (sawa na 4.8% ya eneo lote la Tanzania) ikiwa km² 8,029 ndizo maji ya ndani (hasa Ziwa Tanganyika) na km² 37,037 ndizo nchi kavu. Takriban robo ya eneo la mkoa wa Kigoma hutumika kwa kilimo na ufugaji, karibu nusu ni misitu. Kwa ujumla eneo la mkoa ni tambarare ya juu inayoanza kwenye mita 800 juu ya UB karibu na Ziwa Tanganyika na kupanda hadi mita 1,750. Mito ya kudumu ndani ya mkoa wa K...

UK yawatahadharisha Watanzania Kuhusu Maandamano Ya Tarehe 26/04/2018

                London, Uingereza. Serikali ya Uingereza imewataka wananchi wake wanaoishi hapa nchini kuchukua tahadhari na maandamano ya kisiasa yanayotarajiwa kufanyika Aprili 26. Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo Aprili 24 imesema kwamba kuna raia zaidi ya 75,000 wanaoingia nchini hapa kila mwaka. Hivyo imewatahadharisha kujihusisha na maandamano hayo kwa madai kwamba wanaweza kupata madhara kutoka kwa jeshi la polisi. Katika taarifa hiyo ilitolewa tahadhari kwamba kwa sababu maandamano hayo yalishapigwa marufuku hivyo polisi ni lazima watatumia mabomu ya machozi au silaha za moto. “Hivyo muwe makini sana mnapokuwa kwenye mizunguko yenu muepuke mikusanyiko ya watu au watu wanaoandamana, muda wote muwe mnasikiliza vyombo vya habari, mjue nini kinachoendelea,’’ ilisema taarifa hiyo na kuongeza: “Ikiwa mnahitaji mawasiliano na namba ya dharura ya kupiga haraka ni 112 uliza huduma ya d...

Diamond Amtumia Salamu Ali Kiba Baada ya Kusikia Amefunga Ndoa

From Daimond "Ni Mwendo wa Picha za Suti tu sasa hivi, Maana nisije nikafungua hata kashati nikajikuta Centro...Pole yenu Wa zee wa Gym, Kama Muscat Round hii🤣🤣🤣.... Wadau Nimeambiwa King Kiba kaoa leo...Mfikishieni Salam zangu, za Ndoa njema, na Maisha yenye Furaha, Amani na Baraka tele...🔥🔥🔥 # SanaaImezaliwaUpya "