Skip to main content

KUZAA KILA MWAKA, LIKIZO YA UZAZI VYAZUA MJADALA BUNGENI

SERIKALI imesema hakuna haja ya kubadilisha sheria ya uzazi iliyopo kwa sasa, sababu inampa fursa mwanamke kupumzika kutozaa mara kwa mara na kufuata uzazi wa mpango kama nchi inavyoelekeza na si vinginevyo.

Hayo yamesemwa Bungeni leo, Aprili 18 mjini Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika, wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Sonia Juma Magogo, aliyetaka kufahamu mpango wa serikali wa kutaka kuwasaidia kina mama ambao wanajifungua kabla ya kipindi cha kuruhusiwa kupata miezi mitatu ya mapumziko ili waweze kuwanyonyesha vichanga na kuendelea majuKumu yao ya kazi.

Kwa mujibu wa kanuni za utumishi wa umma za mwaka 2009, mtumishi wa umma anapojifungua hupewa likizo ya malipo ya siku 84, endapo atajifungua zaidi ya mtoto mmoja (mapacha) ataongezewa siku 14 na kuwa jumla ya siku 98,amesema mkuchika

Lakini mtumishi akijifungua mtoto tena kabla ya kutimiza miaka mitatu, atapewa likizo maalum ya wiki sita ili kuhudumia mtoto wake kwa mujibu wa kanuni na baada ya hapo serikali inaweza kumuongezea siku za kupumzika kulingana na ushauri wa daktari.

“Ikumbukwe kwamba, likizo ya uzazi hutolewa mara moja katika kipindi cha miaka mitatu kwa kuzingatia sera ya afya ya mama na mtoto inayosisitiza kulinda na kujenga afya ya mama na mtoto na kuhimiza uzazi wa mpango.

Sheria hizi ni za nchi nzima hivyo zinapaswa ziheshimiwe na kufuatwa kwa watumishi wa serikali na mashirika ya umma.

Aidha, Mbunge Mgila alisema uzazi wa mpango ni makubaliano ya wanandoa ikiwemo lini wazae na kuitaka serikali kubadilisha sheria hiyo ya likizo ambapo Waziri Mkuchika amesema kuzaa baada miaka mitatu inatosha huku akisema wanaume wawahurumie wanawake wanaowazalisha kila mwaka kwani nao wanahitaji kupumzika.

Mkuchika ametoa rai kwa watumishi wa umma au sekta binafsi, kuwa endapo yeyote atanyimwa haki ya likizo ya uzazi aitaarifu wizara husika ili hatua stahiki zichukuliwe dhidi ya mwajiri wake.

Comments

Popular posts from this blog

Historia ya mkoa wa kigoma

 Mkoa wa Kigoma  uko kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye postikodi namba 47000. Umepakana na Burundi na Mkoa wa Kagera upande wa Kaskazini, mikoa ya Shinyanga na Tabora upande wa mashariki na Mkoa wa Rukwa upande wa kusini. Magharibi umepakana na Ziwa Tanganyika penye mpaka na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Viwianishi: 4°53′S 29°40′E / 4.883°S 29.667°E Nchi Tanzania Wilaya 8 Mji mkuu Kigoma Serikali - Mkuu wa Mkoa Emmanuel Maganga Eneo - Mkoa 46,066 km² - Bara 37,037 km² - Maji 8,029 km² Idadi ya wakazi (2012) - 2,127,930 Jiografia Mkoa una eneo la km² 45,066 (sawa na 4.8% ya eneo lote la Tanzania) ikiwa km² 8,029 ndizo maji ya ndani (hasa Ziwa Tanganyika) na km² 37,037 ndizo nchi kavu. Takriban robo ya eneo la mkoa wa Kigoma hutumika kwa kilimo na ufugaji, karibu nusu ni misitu. Kwa ujumla eneo la mkoa ni tambarare ya juu inayoanza kwenye mita 800 juu ya UB karibu na Ziwa Tanganyika na kupanda hadi mita 1,750. Mito ya kudumu ndani ya mkoa wa K...

Stendi ya mabasi ya mikoani Ubungo kuhamishwa kupisha kituo cha mabasi ya Mwendo Kasi

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ipo kwenye majadiliano ya kuhamisha kituo cha Mabasi Yaendayo Haraka (UDART), kilichopo Jangwani na kukipeleka kwenye kituo cha Mabasi yaendayo Mikoani Ubungo (UBT). Hatua hiyo inatokana na eneo hilo la Jangwani kukumbwa na mafuriko ya mara kwa mara hali inayosababisha kuharibika kwa magari hayo. Akizungumza kwenye kikao cha kawaida cha madiwani jana, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita, alisema uamuzi huo umefikiwa ili kunusuru magari hayo yasiendelee kuharibika. Alisema Menejimenti ya Kampuni ya UDART na viongozi wa jiji wapo kwenye majadiliano kuhusu suala hilo ili waweze kufikia mwafaka. “Kwa sasa tupo kwenye majadiliano kwa ajili ya kuhamisha kituo cha mabasi yaendayo kasi(UDART) cha Jangwani tuweze kukipeleka Ubungo kwa sababu eneo la Jangwani limekuwa likikumbwa na mafuriko ya mara kwa mara mvua inaponyesha,” alisema Mwita. Alisema suala hilo linaendelea kufanyiwa kazi na Halmashauri ya Jiji hilo ipo kwenye mchakato wa kupanua Mt...

Mabasi ya Mwendokasi yasitisha huduma zake kwa muda

Kampuni inayotoa huduma katika mradi wa mabasi yaendayo haraka (UDART) imeamua kusitisha usafirishaji wa abiria kwa baadhi ya njia kuanzia saa 6:00 mchana kutokana na kufungwa kwa barabara ya Morogoro eneo la Jangwani kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha.  Hayo yameelezwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano UDART, Deus Bugaywa na kusema wamechukua maamuzi hayo kutokana na maji mengi ya mvua kupita juu ya daraja la Mto Msimbazi Jijini Dar es Salaam hali ambayo inahatarisha usalama wa abiria pamoja na vyombo vya usafirishaji.  "Kwa sasa huduma zinatolewa kwa njia za Mbezi - Kimara, Kimara - Morroco, Kimara - Magomeni Mapipa, Kivukoni - Muhimbili, Gerezani - Kvukoni, na Gerezani - Muhimbili. Huduma kamili zitarejea mara baada ya barabara kufunguliwa", amesema Bugaywa. Kwa upande mwingine, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano UDART, Deus Bugaywa amewaomba radhi wananchi wanaotumia usafiri huo kwa usumbufu ambao utajitokeza kwa namna moja ama ny...