SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, amemtaka mwandishi wa gazeti la Raia Mwema, Paschal Mayala na wahariri wa chombo hicho kufika mbele ya Kamati ya Maadili ya Bunge ili kuhojiwa kwa madai ya kulidhalilisha Bunge.
Ndugai ametoa wito huo leo Aprili 12, 2018 Bungeni mjini Dodoma wakati akitolea maamuzi mwongozo wa Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga, aliouomba Bungeni kulitaka lichukue hatua kwa kile alichokieleza kwamba gazeti hilo limechapisha makala yenye mlengo wa kulidhalilisha Bunge hilo.
Inadaiwa kwamba, Mayala aliandika makala kwenye gazeti hilo toleo la Aprili 9, 2018 iliyosema “Bunge Linajipendekeza kwa Serikali.” Aidha, Ndugai hakutaja wanahabari hao wafike lini mbele ya kamati kwa ajili ya kuhojiwa.
Comments
Post a Comment