Skip to main content

Mwenyekiti Bavicha mbeya ashikiliwa na Polisi

Mbeya. Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) Mkoa wa Mbeya, George Titho amekamatwa na polisi usiku wa manane nyumbani kwake kijijini Kyimo wilayani Rungwe.


Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Mussa Taibu alipoulizwa na MCL Digital kuhusu kukamatwa kiongozi huyo, amesema hana taarifa.


"Sina taarifa hizo, labda nifuatilie lakini jua tu kwamba hali Mbeya ni shwari," amesema Kamanda Taibu.


Katibu wa Chadema Mkoa wa Mbeya, Boid Mwabulanga amesema Titho alikamatwa usiku wa kuamkia Aprili 26, 2018.

Mwabulanga amesema hawajaambiwa sababu za kukamatwa kwa Titho na jitihada za kumwekea dhamana zimegonga mwamba.

"Walikwenda nyumbani kwake saa nane usiku na kuvunja mlango, wakachukua simu zake kisha wakamchukua kwenda naye kituo cha polisi Tukuyu. Tumekwenda asubuhi kumwekea dhamana lakini walikataa,” amesema.

Comments

Popular posts from this blog

Niyonzima Apata Ajali Ya Gari

Haruna Niyonzima KIUNGO wa Simba, Haruna Niyonzima amenusurika katika ajali aliyoipata eneo la Mwenge jijini Dar es Salaam. Niyonzima amepata ajali hiyo juzi baada ya gari lake kupiga bonde na kupoteza mwelekeo wakati akirejea nyumbani kwake. Taarifa zinaeleza Niyonzima raia wa Rwanda alikuwa mwenyewe kwenye gari na akiwa njiani wakati anarejea nyumbani, akakutana na majanga hayo. Jana Championi  juhudi za kumpata Niyonzima aliyetua nchini kuichezea Yanga akitokea APR ya Rwanda na baada ya kumpata alithibitisha kupata ajali na kusema anamshukuru Mungu kwa kuwa haikuwa ajali kubwa. “Gari lilipoteza mwelekeo wakati nikiwa njiani narejea nyumbani na kuingia kwenye msingi. Bahati nzuri sikuwa katika mwendo mkubwa na kuna mtu alikatiza ghafla, nilipojaribu kumkwepa nikapoteza mwelekeo wakati najitahidi kurudi barabarani, nikapiga bonde gari likanishinda nikaingia msingini. “Haukuwa msingi mrefu, baadaye walikuja watu tukalitoa nikaondoka. Nashukuru sikuumia wala yule mtu si...

Wema ampiga dongo Mange Kimambi kuhusu maandamano yake

Wema Sepetu amempiga dongo Mange Kimambi kufuatia maandamano aliyokuwa akiyahamasisha kupitia mitandao ya kijamii akiwataka Watanzania waandamane kutokufanikiwa.  Mange alikuwa akiwashawishi Watanzania kuandamana leo katika maadhimisho wa miaka 54 ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni ishara ya kupinga baadhi ya mambo yanayofanywa na serikali ya awamu ya tano, lakini hata hivyo, maandamano hayo hayajafanyika katika kiwango kilichokuwa kikidhaniwa.  Watu wengi leo walikaa majumbani mwao wakihofia kutoka nje kutokana na polisi kutishia kuwashughulikia wale wote watakaoandamana, hali iliyopelekea baadhi ya watu kukatisha shughuli zao.  Kupitia ukurasa wake wa Instagram Wema amesema kuwa alisitisha safari yake ya kwenda Arusha kutokana na hofu kuwa kungekuwa na maandaamano, kumbe hakuna kitu chochote.  “Watu Tukajua Kuna Maandamano mpaka Safari tukazihairisha… Kumbe hamna kitu… Ila utani tuweke pembeni wengi wetu tulishtushwa… But one thing y...

Rais Magufuli aitangaza Manispaa ya Dodoma kuwa Jiji

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, ameipandisha hadhi Manispaa ya Mji wa Dodoma na kuwa Jiji, huku akimtaja Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma wa sasa kuwa Mkurugenzi wa Jiji hilo jipya. Dkt. Magufuli amesema hayo leo Alhamisi, Aprili 26, 2018 wakati akihutubia wananchi waliojitokeza katika Viwanja vya Jamhuri, Dodoma wakati wa Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kutengeneza Tanzania. “Lengo la Serikali yetu kuhamia Dodoma lipo pale pale, hatuwezi kurudi nyuma. Sasa hivi zaidi ya watumishi 3,800 wameshahamia, mimi nitahamia Dodoma mwaka huu. Dodoma ndio Makao Makuu. Kwa mamlaka mliyonipa, natangaza rasmi kuanzia leo Aprili 26, 2018, Manispaa ya Dodoma itakuwa Jiji la Dodoma, mkurugenzi wake ataanza kuitwa Mkurugenzi wa Jiji”, amesema Dkt. Magufuli. Aidha, Rais Magufuli amesema maandalizi yote ya kisheria yaanze kutumika katika jiji hilo jipya nalitakuwa Jiji la kipekee kwa sababu lipo katikati ya ...