Skip to main content

Sababu ya niyonzima kutokucheza hii hapa

KOCHA wa Simba, Pierre Lechantre amesema ugumu wa mechi wanazokutana nazo kwa sasa ndiyo sababu kubwa inayomfanya kutowatumia kabisa Haruna Niyonzima na Said Ndemla katika mechi mbili zilizopita.

Niyonzima ambaye hivi karibuni alitoka katika kipindi cha majeraha, hajawa sehemu ya kikosi cha Simba ambacho kimecheza dhidi ya Prisons na kushinda mabao 2-0 na dhidi ya Mbeya City waliyoshinda kwa mabao 3-1.

Mechi zote zilichezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Cham­pioni Jumatano, Lechan­tre amesema ameshindwa kuwatumia viungo hao kwenye mechi hizo mbili kwani wapinzani wao wa­likuwa wanakaba sana na kutumia nguvu nyingi.

“Kuhusu Niyonzima kutocheza nilifanya hivyo kwa sababu kwenye mechi hizi mbili ambazo tumecheza na Mbeya City na Prisons, nilibaini kwamba wapinzani wangu wana watu ambao wanacheza kwa nguvu kubwa sana.

“Pia watu wao wanakaba sana hivyo nikaona nisiwa­tumie viungo halisi wa­naocheza nafasi ya kiungo mchezeshaji na nikawapanga watu wengine.

“Kama mechi na Prisons utaona kabisa wapinzani wetu walikuwa wanach­eza kwa kukaba mtu na mtu, sasa hapo ningesema kwamba nitumie viungo wachezeshaji ambao kwenye suala la kukaba siyo wazuri ingekuwa pigo kwetu hivyo nilichofanya ni kuwaweka pembeni tu.

“Lakini kwenye michezo ijayo wanaweza kutumika kwani siyo kila mchezo ambao tutacheza mambo yatakuwa hivihivi,” alisema Lechantre raia wa Ufaransa.

Comments

Popular posts from this blog

Historia ya mkoa wa kigoma

 Mkoa wa Kigoma  uko kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye postikodi namba 47000. Umepakana na Burundi na Mkoa wa Kagera upande wa Kaskazini, mikoa ya Shinyanga na Tabora upande wa mashariki na Mkoa wa Rukwa upande wa kusini. Magharibi umepakana na Ziwa Tanganyika penye mpaka na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Viwianishi: 4°53′S 29°40′E / 4.883°S 29.667°E Nchi Tanzania Wilaya 8 Mji mkuu Kigoma Serikali - Mkuu wa Mkoa Emmanuel Maganga Eneo - Mkoa 46,066 km² - Bara 37,037 km² - Maji 8,029 km² Idadi ya wakazi (2012) - 2,127,930 Jiografia Mkoa una eneo la km² 45,066 (sawa na 4.8% ya eneo lote la Tanzania) ikiwa km² 8,029 ndizo maji ya ndani (hasa Ziwa Tanganyika) na km² 37,037 ndizo nchi kavu. Takriban robo ya eneo la mkoa wa Kigoma hutumika kwa kilimo na ufugaji, karibu nusu ni misitu. Kwa ujumla eneo la mkoa ni tambarare ya juu inayoanza kwenye mita 800 juu ya UB karibu na Ziwa Tanganyika na kupanda hadi mita 1,750. Mito ya kudumu ndani ya mkoa wa K...

UK yawatahadharisha Watanzania Kuhusu Maandamano Ya Tarehe 26/04/2018

                London, Uingereza. Serikali ya Uingereza imewataka wananchi wake wanaoishi hapa nchini kuchukua tahadhari na maandamano ya kisiasa yanayotarajiwa kufanyika Aprili 26. Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo Aprili 24 imesema kwamba kuna raia zaidi ya 75,000 wanaoingia nchini hapa kila mwaka. Hivyo imewatahadharisha kujihusisha na maandamano hayo kwa madai kwamba wanaweza kupata madhara kutoka kwa jeshi la polisi. Katika taarifa hiyo ilitolewa tahadhari kwamba kwa sababu maandamano hayo yalishapigwa marufuku hivyo polisi ni lazima watatumia mabomu ya machozi au silaha za moto. “Hivyo muwe makini sana mnapokuwa kwenye mizunguko yenu muepuke mikusanyiko ya watu au watu wanaoandamana, muda wote muwe mnasikiliza vyombo vya habari, mjue nini kinachoendelea,’’ ilisema taarifa hiyo na kuongeza: “Ikiwa mnahitaji mawasiliano na namba ya dharura ya kupiga haraka ni 112 uliza huduma ya d...

Diamond Amtumia Salamu Ali Kiba Baada ya Kusikia Amefunga Ndoa

From Daimond "Ni Mwendo wa Picha za Suti tu sasa hivi, Maana nisije nikafungua hata kashati nikajikuta Centro...Pole yenu Wa zee wa Gym, Kama Muscat Round hii🤣🤣🤣.... Wadau Nimeambiwa King Kiba kaoa leo...Mfikishieni Salam zangu, za Ndoa njema, na Maisha yenye Furaha, Amani na Baraka tele...🔥🔥🔥 # SanaaImezaliwaUpya "