Skip to main content

Salah anatamani kutwaa tuzo ya mfungaji bora

Mshambuliaji wa klabu ya Liverpool, Mohamed Salah amesisitiza kuwa lengo lake kuu msimu huu ni kutwaa tuzo ya mfungaji bora huku akiamini kuwa bado anavitu vingi vya kuonyesha Ligi kuu ya Uingereza na wala hafanyi yote kwa sababu ya kupata nafasi kujiunga ndani ya kikosi cha Chelsea kama inavyoelezwa.

Salah ambaye anajumla ya mabao 30 kwenye ligi kuu ya Uingereza msimu huu akimzidi mchezaji wa timu ya Tottenham, Harry Kane zaidi ya manne huku ikiwa imesalia michezo minne pekee kabla ya kumalizika kwa ligi hiyo.

Kupitia mahojiano na Sky Sports mara baada ya mchezo wao na West Brom, Salah amesema “Unaweza kuona michezo kadhaa iliyopita, wachezaji wanajaribu kunisaidia sana kufunga magoli, kwasababu wanafahamu kuwa nipo katika mbio za kuwania kiatu cha dhahabu lakini mwisho wa siku ni zawadi ya mtu binafsi lakini pia kufanya hivyo huisaidia timu,”amesema Salah.

Mo Salah ameongeza “Kwa namna tunavyocheza hakika inavutia na unaweza kuona mashabiki wakiwa na furaha kiasi ambacho najisikia vizuri kwa hilo nadhani wanahitaji kuniona nikishinda kitu fulani.

” “Tumesaliwa na michezo minne, hili lipo wazi ninacheza kwahili tangu awali lakini pia marazote ni kwaajili ya timu na nahitaji kufunga magoli mengi kwaajili ya timu.”

Takwimu zikionyesha kuwa kwenye kila mchezo ana goli moja la ugenini ligi ya Uingereza rekodi ambayo iliwahi kuwekwa na wachezaji kama, Alan Shearer msimu wa mwaka (95/96), Cristiano Ronaldo mwaka (07/08) na Luis Suarez mwaka (13/14), hata hivyo inaelezwa kuwa Salah husema kuwa timu ni lazima kupata matokeo kwanza licha ya kuwa na hamu ya kuitawala nafasi ya kwanza ya ufungaji.

Comments

Popular posts from this blog

Historia ya mkoa wa kigoma

 Mkoa wa Kigoma  uko kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye postikodi namba 47000. Umepakana na Burundi na Mkoa wa Kagera upande wa Kaskazini, mikoa ya Shinyanga na Tabora upande wa mashariki na Mkoa wa Rukwa upande wa kusini. Magharibi umepakana na Ziwa Tanganyika penye mpaka na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Viwianishi: 4°53′S 29°40′E / 4.883°S 29.667°E Nchi Tanzania Wilaya 8 Mji mkuu Kigoma Serikali - Mkuu wa Mkoa Emmanuel Maganga Eneo - Mkoa 46,066 km² - Bara 37,037 km² - Maji 8,029 km² Idadi ya wakazi (2012) - 2,127,930 Jiografia Mkoa una eneo la km² 45,066 (sawa na 4.8% ya eneo lote la Tanzania) ikiwa km² 8,029 ndizo maji ya ndani (hasa Ziwa Tanganyika) na km² 37,037 ndizo nchi kavu. Takriban robo ya eneo la mkoa wa Kigoma hutumika kwa kilimo na ufugaji, karibu nusu ni misitu. Kwa ujumla eneo la mkoa ni tambarare ya juu inayoanza kwenye mita 800 juu ya UB karibu na Ziwa Tanganyika na kupanda hadi mita 1,750. Mito ya kudumu ndani ya mkoa wa K...

Stendi ya mabasi ya mikoani Ubungo kuhamishwa kupisha kituo cha mabasi ya Mwendo Kasi

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ipo kwenye majadiliano ya kuhamisha kituo cha Mabasi Yaendayo Haraka (UDART), kilichopo Jangwani na kukipeleka kwenye kituo cha Mabasi yaendayo Mikoani Ubungo (UBT). Hatua hiyo inatokana na eneo hilo la Jangwani kukumbwa na mafuriko ya mara kwa mara hali inayosababisha kuharibika kwa magari hayo. Akizungumza kwenye kikao cha kawaida cha madiwani jana, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita, alisema uamuzi huo umefikiwa ili kunusuru magari hayo yasiendelee kuharibika. Alisema Menejimenti ya Kampuni ya UDART na viongozi wa jiji wapo kwenye majadiliano kuhusu suala hilo ili waweze kufikia mwafaka. “Kwa sasa tupo kwenye majadiliano kwa ajili ya kuhamisha kituo cha mabasi yaendayo kasi(UDART) cha Jangwani tuweze kukipeleka Ubungo kwa sababu eneo la Jangwani limekuwa likikumbwa na mafuriko ya mara kwa mara mvua inaponyesha,” alisema Mwita. Alisema suala hilo linaendelea kufanyiwa kazi na Halmashauri ya Jiji hilo ipo kwenye mchakato wa kupanua Mt...

Mabasi ya Mwendokasi yasitisha huduma zake kwa muda

Kampuni inayotoa huduma katika mradi wa mabasi yaendayo haraka (UDART) imeamua kusitisha usafirishaji wa abiria kwa baadhi ya njia kuanzia saa 6:00 mchana kutokana na kufungwa kwa barabara ya Morogoro eneo la Jangwani kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha.  Hayo yameelezwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano UDART, Deus Bugaywa na kusema wamechukua maamuzi hayo kutokana na maji mengi ya mvua kupita juu ya daraja la Mto Msimbazi Jijini Dar es Salaam hali ambayo inahatarisha usalama wa abiria pamoja na vyombo vya usafirishaji.  "Kwa sasa huduma zinatolewa kwa njia za Mbezi - Kimara, Kimara - Morroco, Kimara - Magomeni Mapipa, Kivukoni - Muhimbili, Gerezani - Kvukoni, na Gerezani - Muhimbili. Huduma kamili zitarejea mara baada ya barabara kufunguliwa", amesema Bugaywa. Kwa upande mwingine, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano UDART, Deus Bugaywa amewaomba radhi wananchi wanaotumia usafiri huo kwa usumbufu ambao utajitokeza kwa namna moja ama ny...