Siku moja tu baada ya picha za mwanamke mmoja kusambaa mitandaoni akitolewa chupi kanisani na jamaa aliyedaiwa kuwa pasta, mwanamke huyu amevunja kimya.
Wengi walikishutumu kisa hicho huku uozo katika jamii ukibanika wazi. Baadhi wakidai kuwa mapasta hufanya lolote na hata kuwadhulumu na kukiuka haki za waumini kwa jina la kusuluhishia matatizo yao.
‘’ Hii ni movie wala si kanisa kama wengi wanavyodai, tafadhali komeni kueneza habari za uongo. Mimi ni muigizaji na ni jukumu langu kutoa lesoni kamili kwa ulimwengu.’’ Alibainisha Mwanamke muigizaji ambaye sasa ametambulika kama Piesie Asamoah Gifty kupitia kwa mtandao wake wa Facebook.
Jaridala TUKO.co.ke limeweza kuthibitisha kuwa video hiyo ya kuigiza kina mada ‘Pastor Blinks’ na kitazinduliwa hivi karibuni.
Mwandishi wa mchezo huo Trus Pleroma Nyowikech alivilaumu vikali vyombo vya habari kwa kueneza habari hiyo.
Mwanamke huyo ameeleza kuwa huo ulikuwa mchezo wa kuigiza.
‘’ Kwa wale ambao hawakuamini nilipozichapisha baadhi ya picha hizi. Huyu ni msanii wa ucheshi wa Ghana katika mchezo ‘Pastor Blinks’. Hebu tazama tena! Kutana na Mensah Mark, (mhusika wa pastor blink) katika mchezo huu.'' Aliandika.
Kabla ukweli huu kubainika, wengi walimshutumu vikli ‘pasta’ huyo aliyeaminika kuwavulia chupi wanawake na kuwanyoa makwapa kama njia ya kuwabariki.
Comments
Post a Comment