Rais Donald Trump anatarajia kukutana na rais wa Korea Kusini Moon Jae In ifikapo 22 Mei. Viongozi hao wawili watakutana katika ikulu ya White House nchini Marekani. Msemaji wa White House Sarah Sanders ametoa maelezo kuhusu mkutano huo na kusema kuwa Korea Kusini ina uhusiano mzuri na Marekani. Trump ambae natarajia kukutana na Moon kwa mara ya tatu sasa,anaamini mkutano huo utasaidia katika kudumisha mahusiano kati ya mataifa hayo amwili. Trump vilevile anatarajia kukutana na Kim Jong Un hivi karibuni.