Rais John Magufuli ameiomba Serikali ya Denmark kusaidia ujenzi wa kipande cha barabara ya kilomita 11 katika Mkoa wa Iringa ili kuwezesha malori kutopita katikati ya mji huo ikiwa ni pamoja na kupunguza ajali zinazotokea.
Rais Magufuli ombi hilo wakati akizindua barabara ya Iyovi – Iringa – Mafinga yenye urefu wa kilomita 218 iliyojengwa kwa mkopo nafuu kutoka serikali ya Denmark na kugharimu Sh283 bilioni.
Akitoa maelezo wakati akiomba msaada huo Dk. Magufuli amesema mpango huo ulikuwepo tangu alipokuwa wizara ya ujenzi na kufafanua kwamba malori yanayopita katikati ya mji wa Iringa yamekuwa yakisababisha ajali ndani ya mji wa huo.
“Nakuomba Balozi, hili mlichukue kama la urgent, mkitusaidia kama mkopo sisi tuko tayari, mkitupa kama msaada tutashukuru zaidi. Kwa hiyo tunaomba utufikishie hili, ikiwezekana barabara hiyo tutaiita Pamela Road,” amesema
Mbali na hayo Rais ameweka wazi kwamba "Ujenzi wa barabara hii umegharimu bilioni 283.71 nimekopa kutoka Denmark, mbali na kufadhili mradi huu ilisaidia kukarabati barabara za Chalinze - Mlandizi, Chalinze - Segera, kwa niaba ya watanzania natumia fursa hii kutoa shukrani zangu".
Comments
Post a Comment