Watu watatu wamefariki papo hapo baada ya kugongwa na gari aina ya basi Frester lenye namba za usajili T.720 DEV eneo la Katongo kata ya Rulanda wilayani Muleba mkoani Kagera asubuhi hii ya leo
Miili haijatambulika watu hao ni vijana walikuwa wakienda madrasa ambapo basi hilo lilikuwa likitokea Bukoba kwenda Mwanza
Kwa mujibu wa abiria waliokuwa kwenye basi hilo wamesema dreva alitaka kumkwepa mwendesha bodaboda na kuwaparamia vijana hao akiwemo huyo bodaboda na kusababisha gari kupinduka
Aidha abiria waliojeruhiwa wanaokolewa na wenzao kwani viungo vya miili vimenasa kwenye vyuma huku zikifanyika jitihada za kuwapeleka kituo cha afya kaigara na hospitali ya Rubya wilayani Muleba.
Hali ya hewa katika eneo hilo kulikuwa pia na ukungu ulioambatana na mvua inadaiwa basi lilikuwa mwendo kasi likitangulia mengine yaliyokuwa yakienda mikoani.
Comments
Post a Comment