Binti wa miaka 20 ambaye jina lake halikutajwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi Temeke jijini Dar es salaam kwa tuhuma za kumuua mtoto wa miaka miwili, ambaye ametajwa ni mdogo wake na kisha kumficha uvunguni mwa kitanda huko nyumbani kwao Kigamboni jijini Dar es salaam.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Temeke Emmanuel Lukula amesema tukio hilo limetokea Jumatatu ya April 23, ambapo binti huyo alimchoma na kitu chenye ncha kali sehemu ya kitovu mtoto huyo na kumlaza kifudi fudi, kisha kutokomea kwa mpenzi wake.
“Ni kweli tukio hilo limetokea,aliyefanya hilo tukio ni binti wa miaka 20 ambaye ni ndugu wa mama wa marehemu, alimchoma huyo mtoto na kumlaza kifudifudi uvunguni kisha akaondoka kwa mwanaume anayedaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi, na baada ya mama wa mtoto kurudi kazini hakumkuta nyumbani”, amesema Kamanda Lukula.
Kamanda Lukula ameendelea kueleza kwamba baada ya hapo mama alitoa taarifa polisi, na baada ya uchunguzi walimkamata binti huyo na kuonyesha mahali alipomficha mtoto huyo, na mpaka sasa anashikiliwa jeshi la polisi ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.
Mkoa wa Kigoma uko kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye postikodi namba 47000. Umepakana na Burundi na Mkoa wa Kagera upande wa Kaskazini, mikoa ya Shinyanga na Tabora upande wa mashariki na Mkoa wa Rukwa upande wa kusini. Magharibi umepakana na Ziwa Tanganyika penye mpaka na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Viwianishi: 4°53′S 29°40′E / 4.883°S 29.667°E Nchi Tanzania Wilaya 8 Mji mkuu Kigoma Serikali - Mkuu wa Mkoa Emmanuel Maganga Eneo - Mkoa 46,066 km² - Bara 37,037 km² - Maji 8,029 km² Idadi ya wakazi (2012) - 2,127,930 Jiografia Mkoa una eneo la km² 45,066 (sawa na 4.8% ya eneo lote la Tanzania) ikiwa km² 8,029 ndizo maji ya ndani (hasa Ziwa Tanganyika) na km² 37,037 ndizo nchi kavu. Takriban robo ya eneo la mkoa wa Kigoma hutumika kwa kilimo na ufugaji, karibu nusu ni misitu. Kwa ujumla eneo la mkoa ni tambarare ya juu inayoanza kwenye mita 800 juu ya UB karibu na Ziwa Tanganyika na kupanda hadi mita 1,750. Mito ya kudumu ndani ya mkoa wa K...
Comments
Post a Comment