STAA mkali wa filamu Bongo, Irene Uwoya na baby wake Abdul Chende ‘Dogo Janja’ wamefungukia dhamira yao ya kuihama nyumba waliyokuwa wakiishi na marehemu Agness Gerald ‘Masogange’ iliyopo Makongo Juu jijini Dar wakidai kuwa, hawatakuwa na amani.
Akizungumza na Risasi Jumamosi kwa niaba ya mkewe, Dogo Janja alisema kuwa hawawezi kuendelea kuishi hapo tena kwa sababu kwao itakuwa ni majonzi kila siku na hiyo ni kutokana na ukaribu waliokuwa nao kwa Masogange.
“Kwa kweli mimi na mke wangu hatuwezi tena kuendelea kuishi Makongo Juu kwenye ile nyumba maana kwetu itakuwa ni simanzi tuu, Masogange alikuwa ni mtu wetu wa karibu sana na tulikuwa tukifanya vitu vingi pamoja, pia mke wangu atakuwa na huzuni sana akiendelea kuishi pale,” alisema Dogo Janja.
Comments
Post a Comment