RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli ameridhia na kuwapandisha vyeo maofisa 28 wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kuanzia leo Aprili 12, 2018 huku akimbadilisha Mpambe wake Kanali Mkeremi ambaye amempandisha cheo na atapangiwa kazi nyingine jeshini.
Aidha, Rais pia amekukubali kumpandisha cheo kutoka Luteni Kanali kuwa kanali D.P.M Murunga na kuwa mpambe wa Rais akichukua nafasi ya Mkeremi.
Akitoa taarifa ya uteuzi huo, Mkuu wa Majeshi, Jenerali Venancy Mabeyo amesema maofisa walioteuliwa wanakwenda kuimarisha safu za utendaji kazi kijeshi na kwamba maofisa wote hao watavalishwa vyeo vyao Ijumaa hii katika makamo makuu ya Jeshi Upanga Jijini Dar es salaam.
Katika uteuzi huo Rais Magufuli amewapandisha vyeo maofisa wa ngazi mbalimbali Jeshini ikiwa ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma Kanali M E Gaguti ambaye sasa anapanda cheo na kuwa Brigedia Jenerali na kurejeshwa Jeshini.
Comments
Post a Comment