Skip to main content

Diva the bawse Atakiwa Kumlipa Michael Lukindo Mil.50


Msanii wa Bongo fleva na mtangazaji wa Cloud Fm ,Diva Gissele Malinzi maarufu kama "Diva the bawse" ametakiwa kuomba radhi pamoja na kulipa faini ya Tsh.Milioni 50 kwa kosa la kumdhalilisha msanii mwenzake ambaye alikuwa mtangazaji mwenza wa Cloud Fm ,Michael Lukindo. 

Diva amepewa agizo hilo na taasisi ya wanasheria ya "East Woods Attorney" ambako Michael Lukindo aliwasilisha madai yake ya kudhalilishwa. 

Picha liko hivi 
Siku chache zilizopita Michael Lukindo alifanya mahojiano na XXL ya Clouds Fm na alikuwa anatambulisha nyimbo yake mpya ya " Basi Iwe" lakini Kwenye mahojiano hayo alifunguka amewahi kuwa Kwenye Mahusiano na Diva. 

Baada ya kusikia taarifa hizo Diva alitumia ukurasa wake wa Instagram na kumwaga povu zito na kukataa kata kata kama yupo Kwenye Mahusiano ya kimapenzi na Michael Lukindo. 

Baada ya Tetesi hizo kusambaa Soudy Brown alimsaka Michael ambaye alikiri kuwa alikuwepo Kwenye Mahusiano na Diva lakini walifanya siri na mpaka sasa Diva hayupo tayari kuzungumzia hayo mahusiano. 

Baada ya kusikia maneno hayo Diva ambaye kwa muda huo alikuwa studio alimtolea matusi mazito Michael Lukindo: 

“Wewe mata** unikome shika adabu yako umeshawahi kuwa na Mahusiano na mimi lini na wapi?na nilikwambia kabisa kwamba nimekushtaki I have defamation letter for you utajifunza kufunga huo mdomo wako sitaki mambo ya kise*** k*** la mama ako umeenda umemzungumzia Jokate on the same same thing haukutosheka ukamuandika Miriam Odemba kuwa una Mahusiano naye sasahivi unataka kwangu mimi kunitafutia kiki sasa mimi ntakukomesha nimeshakushtaki”. 

"East Woods Attorney" wamemwamndikia barua Diva ambapo wamemtaka amwombe msamaha mteja wao Michael Lukindo pia amlipe Tsh .Milioni 50 . Diva ametakiwa kufanya hayo ndani ya siku 14 kuanzia tarehe 19 April ,2018.Akishindwa kufanya hayo hatua zaidi za kisheria zitachukuliwa 

Hii hapa barua aliyoadnikiwa Diva na wanasheri wa Michael Lukindo. 


Comments

Popular posts from this blog

Historia ya mkoa wa kigoma

 Mkoa wa Kigoma  uko kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye postikodi namba 47000. Umepakana na Burundi na Mkoa wa Kagera upande wa Kaskazini, mikoa ya Shinyanga na Tabora upande wa mashariki na Mkoa wa Rukwa upande wa kusini. Magharibi umepakana na Ziwa Tanganyika penye mpaka na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Viwianishi: 4°53′S 29°40′E / 4.883°S 29.667°E Nchi Tanzania Wilaya 8 Mji mkuu Kigoma Serikali - Mkuu wa Mkoa Emmanuel Maganga Eneo - Mkoa 46,066 km² - Bara 37,037 km² - Maji 8,029 km² Idadi ya wakazi (2012) - 2,127,930 Jiografia Mkoa una eneo la km² 45,066 (sawa na 4.8% ya eneo lote la Tanzania) ikiwa km² 8,029 ndizo maji ya ndani (hasa Ziwa Tanganyika) na km² 37,037 ndizo nchi kavu. Takriban robo ya eneo la mkoa wa Kigoma hutumika kwa kilimo na ufugaji, karibu nusu ni misitu. Kwa ujumla eneo la mkoa ni tambarare ya juu inayoanza kwenye mita 800 juu ya UB karibu na Ziwa Tanganyika na kupanda hadi mita 1,750. Mito ya kudumu ndani ya mkoa wa K...

Stendi ya mabasi ya mikoani Ubungo kuhamishwa kupisha kituo cha mabasi ya Mwendo Kasi

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ipo kwenye majadiliano ya kuhamisha kituo cha Mabasi Yaendayo Haraka (UDART), kilichopo Jangwani na kukipeleka kwenye kituo cha Mabasi yaendayo Mikoani Ubungo (UBT). Hatua hiyo inatokana na eneo hilo la Jangwani kukumbwa na mafuriko ya mara kwa mara hali inayosababisha kuharibika kwa magari hayo. Akizungumza kwenye kikao cha kawaida cha madiwani jana, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita, alisema uamuzi huo umefikiwa ili kunusuru magari hayo yasiendelee kuharibika. Alisema Menejimenti ya Kampuni ya UDART na viongozi wa jiji wapo kwenye majadiliano kuhusu suala hilo ili waweze kufikia mwafaka. “Kwa sasa tupo kwenye majadiliano kwa ajili ya kuhamisha kituo cha mabasi yaendayo kasi(UDART) cha Jangwani tuweze kukipeleka Ubungo kwa sababu eneo la Jangwani limekuwa likikumbwa na mafuriko ya mara kwa mara mvua inaponyesha,” alisema Mwita. Alisema suala hilo linaendelea kufanyiwa kazi na Halmashauri ya Jiji hilo ipo kwenye mchakato wa kupanua Mt...

Mabasi ya Mwendokasi yasitisha huduma zake kwa muda

Kampuni inayotoa huduma katika mradi wa mabasi yaendayo haraka (UDART) imeamua kusitisha usafirishaji wa abiria kwa baadhi ya njia kuanzia saa 6:00 mchana kutokana na kufungwa kwa barabara ya Morogoro eneo la Jangwani kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha.  Hayo yameelezwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano UDART, Deus Bugaywa na kusema wamechukua maamuzi hayo kutokana na maji mengi ya mvua kupita juu ya daraja la Mto Msimbazi Jijini Dar es Salaam hali ambayo inahatarisha usalama wa abiria pamoja na vyombo vya usafirishaji.  "Kwa sasa huduma zinatolewa kwa njia za Mbezi - Kimara, Kimara - Morroco, Kimara - Magomeni Mapipa, Kivukoni - Muhimbili, Gerezani - Kvukoni, na Gerezani - Muhimbili. Huduma kamili zitarejea mara baada ya barabara kufunguliwa", amesema Bugaywa. Kwa upande mwingine, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano UDART, Deus Bugaywa amewaomba radhi wananchi wanaotumia usafiri huo kwa usumbufu ambao utajitokeza kwa namna moja ama ny...