Mwanaume mmoja ambaye anadaiwa kuwa kiongozi wa kidini nchini India na kudai kuwa na mamilioni ya waumini dunia nzima, amehukumiwa kifungo cha maisha jela.
Mwanaume huyo Asaram Bapu ambaye anatajwa kuwa na umri wa miaka 77 amehukumiwa kifungo cha maisha kwa kosa la kumbaka mtoto wa kike wa umri wa miaka 16.
Bapu anaripotiwa kufanya kitendo hicho mwaka 2013 na anatuhumiwa mara nyingi kufanya vitendo hivyo vya ubakaji.
Comments
Post a Comment