BAADA ya hivi karibuni staa wa filamu, Wema Sepetu kueleza maneno aliyoelezwa na aliyekuwa msanii wa filamu, marehemu Steven Kanumba enzi za uhai wake kwamba hataki kabisa mama yake mzazi, Flora Mtegoa aigize, mzazi huyo ameibuka na kufungukia ishu hiyo.
Akipiga stori na Za Motomoto News, mama Kanumba alisema mwanaye huyo alisema hayo kwa sababu alikuwa akimtunza na kumlipa mshahara kama mfanyakazi lakini kwa sasa hayupo hivyo ndiyo maana ameingia kwenye sanaa ya uigizaji kwa kuwa bila hivyo angegeuka ombaomba jambo ambalo halipendezi.
“Kanumba alisema hayo kwa kuwa alikuwa ananitunza yaani ananinunulia vyakula na kunilipa mshahara kila mwezi kama mfanyakazi lakini sasa hayupo, je Wema alitaka nishike bakuli nikaombe barabarani au? Maana kulima siwezi hivyo naona tu bora niigize ili niweze kujikimu kimaisha,” alisema mama Kanumba
Comments
Post a Comment