Skip to main content

Meneja TPA kortini kwa tuhuma za umiliki wa nyumba 23

MENEJA Uhasibu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Prosper Kimaro, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam akikabiliwa na mashtaka ya kuwa na mali zisizolingana na kipato chake.

Akisomewa mashtaka jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, aliyepangiwa kusikiliza kesi hiyo.

Kimaro anadaiwa kumiliki nyumba 23, viwanja vitatu na magari saba vyote vikiwa na thamani ya Sh. bilioni 1.4.

Mawakili wa Serikali, Vitalis Peter akisaidiana na Lilian Wiliam, walidai kuwa katika tarehe tofauti kati ya mwaka 2012 na 2016, wilayani Temeke, Dar es Salaam, mshtakiwa akiwa mtumishi wa umma katika nafasi ya Meneja Uhasibu wa TPA, alikutwa na mali zisizoelezeka. Mali hizo, kwa mujibu wa mawakili hao, ni nyumba mbili zilizoko mtaa wa Uwazi, Temeke zenye thamani ya Sh, 123,273,253 na nyumba moja iliyopo Yombo Vituka yenye thamani ya Sh. 12,956,000.

Peter alidai kuwa mshtakiwa alikutwa akimiliki nyumba 23 na viwanja vitatu vyote vikiwa na thamani ya Sh. 1,178,370,324.

"Mheshimiwa Hakimu mshtakiwa alikuwa na magari saba yakiwamo Toyota LandCruiser yenye namba za usajili T 395 DEJ lenye thamani ya Sh. 180,131,815, Mitsubishi yenye namba za usajili, T 506 CMT ya Sh. 38,464,861, Massey Ferguson yenye namba za usajili T 838 CHH ya Sh. 24,469,060.50, Trela lenye namba za usajili T 383 CNZ la Sh. milioni 4.5, Toyota Harrier yenye namba za usajili T 338 CVX ya Sh. 35,860,617.30, Trela lenye namba za usajili T 938 CVB la Sh. milioni 4.8 na Massey Ferguson yenye thamani ya Sh.19, 138,324.44." alidai Peter wakati akimsomea mashtaka kigogo huyo.

Alidai kuwa mali zote alizokutwa nazo mshtakiwa hazilingani na kipato chake cha zamani na cha sasa.Mshtakiwa alikana mashtaka hayo.

Upande wa Jamhuti ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na haukuwa na pingamizi la dhamana.

Hakimu Simba alisema mshtakiwa atakuwa nje kwa dhamana kwa kuwa na wadhamani wawili watakaowasilisha hati za mali isiyohamishika yenye thamani ya Sh. milioni 200 kila mmoja na pia awasilishe hati zake za kusafiria mahakamani.

Hata hivyo, hadi Nipashe inaondoka mahakamani hapo, mshtakiwa alikuwa hajatimiza masharti ya dhamana. Kesi hiyo imepangwa kutajwa Mei 3, mwaka huu.

Comments

Popular posts from this blog

Historia ya mkoa wa kigoma

 Mkoa wa Kigoma  uko kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye postikodi namba 47000. Umepakana na Burundi na Mkoa wa Kagera upande wa Kaskazini, mikoa ya Shinyanga na Tabora upande wa mashariki na Mkoa wa Rukwa upande wa kusini. Magharibi umepakana na Ziwa Tanganyika penye mpaka na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Viwianishi: 4°53′S 29°40′E / 4.883°S 29.667°E Nchi Tanzania Wilaya 8 Mji mkuu Kigoma Serikali - Mkuu wa Mkoa Emmanuel Maganga Eneo - Mkoa 46,066 km² - Bara 37,037 km² - Maji 8,029 km² Idadi ya wakazi (2012) - 2,127,930 Jiografia Mkoa una eneo la km² 45,066 (sawa na 4.8% ya eneo lote la Tanzania) ikiwa km² 8,029 ndizo maji ya ndani (hasa Ziwa Tanganyika) na km² 37,037 ndizo nchi kavu. Takriban robo ya eneo la mkoa wa Kigoma hutumika kwa kilimo na ufugaji, karibu nusu ni misitu. Kwa ujumla eneo la mkoa ni tambarare ya juu inayoanza kwenye mita 800 juu ya UB karibu na Ziwa Tanganyika na kupanda hadi mita 1,750. Mito ya kudumu ndani ya mkoa wa K...

Stendi ya mabasi ya mikoani Ubungo kuhamishwa kupisha kituo cha mabasi ya Mwendo Kasi

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ipo kwenye majadiliano ya kuhamisha kituo cha Mabasi Yaendayo Haraka (UDART), kilichopo Jangwani na kukipeleka kwenye kituo cha Mabasi yaendayo Mikoani Ubungo (UBT). Hatua hiyo inatokana na eneo hilo la Jangwani kukumbwa na mafuriko ya mara kwa mara hali inayosababisha kuharibika kwa magari hayo. Akizungumza kwenye kikao cha kawaida cha madiwani jana, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita, alisema uamuzi huo umefikiwa ili kunusuru magari hayo yasiendelee kuharibika. Alisema Menejimenti ya Kampuni ya UDART na viongozi wa jiji wapo kwenye majadiliano kuhusu suala hilo ili waweze kufikia mwafaka. “Kwa sasa tupo kwenye majadiliano kwa ajili ya kuhamisha kituo cha mabasi yaendayo kasi(UDART) cha Jangwani tuweze kukipeleka Ubungo kwa sababu eneo la Jangwani limekuwa likikumbwa na mafuriko ya mara kwa mara mvua inaponyesha,” alisema Mwita. Alisema suala hilo linaendelea kufanyiwa kazi na Halmashauri ya Jiji hilo ipo kwenye mchakato wa kupanua Mt...

Mabasi ya Mwendokasi yasitisha huduma zake kwa muda

Kampuni inayotoa huduma katika mradi wa mabasi yaendayo haraka (UDART) imeamua kusitisha usafirishaji wa abiria kwa baadhi ya njia kuanzia saa 6:00 mchana kutokana na kufungwa kwa barabara ya Morogoro eneo la Jangwani kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha.  Hayo yameelezwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano UDART, Deus Bugaywa na kusema wamechukua maamuzi hayo kutokana na maji mengi ya mvua kupita juu ya daraja la Mto Msimbazi Jijini Dar es Salaam hali ambayo inahatarisha usalama wa abiria pamoja na vyombo vya usafirishaji.  "Kwa sasa huduma zinatolewa kwa njia za Mbezi - Kimara, Kimara - Morroco, Kimara - Magomeni Mapipa, Kivukoni - Muhimbili, Gerezani - Kvukoni, na Gerezani - Muhimbili. Huduma kamili zitarejea mara baada ya barabara kufunguliwa", amesema Bugaywa. Kwa upande mwingine, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano UDART, Deus Bugaywa amewaomba radhi wananchi wanaotumia usafiri huo kwa usumbufu ambao utajitokeza kwa namna moja ama ny...