RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, ameipandisha hadhi Manispaa ya Mji wa Dodoma na kuwa Jiji, huku akimtaja Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma wa sasa kuwa Mkurugenzi wa Jiji hilo jipya.
Dkt. Magufuli amesema hayo leo Alhamisi, Aprili 26, 2018 wakati akihutubia wananchi waliojitokeza katika Viwanja vya Jamhuri, Dodoma wakati wa Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kutengeneza Tanzania.
“Lengo la Serikali yetu kuhamia Dodoma lipo pale pale, hatuwezi kurudi nyuma. Sasa hivi zaidi ya watumishi 3,800 wameshahamia, mimi nitahamia Dodoma mwaka huu. Dodoma ndio Makao Makuu. Kwa mamlaka mliyonipa, natangaza rasmi kuanzia leo Aprili 26, 2018, Manispaa ya Dodoma itakuwa Jiji la Dodoma, mkurugenzi wake ataanza kuitwa Mkurugenzi wa Jiji”, amesema Dkt. Magufuli.
Aidha, Rais Magufuli amesema maandalizi yote ya kisheria yaanze kutumika katika jiji hilo jipya nalitakuwa Jiji la kipekee kwa sababu lipo katikati ya Tanzania”.
Comments
Post a Comment