Skip to main content

Serikali Yataifisha Basi na Magari ya Kifahari

Serikali imetaifisha dhahabu ya mabilioni ya shilingi na magari ya kifahari kutokana na wahusika wake kukamatwa na kuhukumiwa kwa makosa ya rushwa katika mwaka huu wa fedha.

Pia imetaifisha, pikipiki, mafuta, mashine za kuhesabia fedha na basi la abiria lililokuwa linatumika kusafirisha meno ya tembo.

Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Paramagamba Kabudi, aliyasema hayo jana alipowasilisha bungeni mjini hapa hotuba ya makadirio ya wizara yake kwa mwaka ujao wa fedha.

Alibainisha kuwa katika mwaka huu wa fedha, mali zilizotaifishwa kwa ujumla wake zinakadiriwa kuwa na thamani ya Sh. bilioni 5.685. Waziri huyo alisema Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ilipokea majalada 683 ya tuhuma za rushwa kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (Takukuru).

Prof. Kabudi alisema kati ya hayo, majalada 288 yaliandaliwa hati za mashtaka na 275 yalirudishwa Takukuru kwa uchunguzi zaidi.

Alisema majalada 115 yako katika hatua mbalimbali yakifanyiwa kazi na mengine matano yalifungwa.

"Washtakiwa waliotiwa hatiani walipewa adhabu mbalimbali zikiwamo vifungo, faini na mali kutaifishwa ambapo jumla ya Sh. bilioni 4.484 zilitozwa kama faini kutoka kwa washtakiwa," alisema na kuongeza: "Mali zilizotaifishwa ni pamoja na kilogramu 24.5 za dhahabu zenye thamani ya Sh. bilioni 2.012 na fedha za kigeni kutoka mataifa 15 zenye thamani ya Sh.milioni 908.092. "Mali zingine zilizotaifishwa ni magari matano ya kifahari aina ya Range Rover Vogue na moja aina ya Audi yaliyokamatwa katika Bandari ya Dar es Salaam yakisafirishwa kama nguo za mitumba, pikipiki 34, mafuta, mashine za kuhesabia fedha na basi la abiria lililokuwa linasarifirisha meno ya tembo."

Prof. Kabudi alisema mwaka huu wa fedha pia mali za vyama vya ushirika vya Mwanza (Nyanza Cooperative Union) na Shinyanga (Shirecu) zikiwamo nyumba, viwanja na viwanda, zimerejeshwa serikalini kutoka mikononi mwa watu ambao walizichukua bila kufuata utaribu wa kisheria.

Waziri huyo pia alisema mwaka huu wa fedha kulikuwa na mashauri sita yanayohusu ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi yaliyoshughulikiwa.

Alisema kuwa kati yake, mashauri manne yalikamilika kwa watuhumiwa kutiwa hatiani na kuhukumiwa adhabu za kifungo cha kati ya miaka minne hadi 20 na mashauri mawili yaliyobaki yanaendelea kusikilizwa.

Comments

Popular posts from this blog

Historia ya mkoa wa kigoma

 Mkoa wa Kigoma  uko kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye postikodi namba 47000. Umepakana na Burundi na Mkoa wa Kagera upande wa Kaskazini, mikoa ya Shinyanga na Tabora upande wa mashariki na Mkoa wa Rukwa upande wa kusini. Magharibi umepakana na Ziwa Tanganyika penye mpaka na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Viwianishi: 4°53′S 29°40′E / 4.883°S 29.667°E Nchi Tanzania Wilaya 8 Mji mkuu Kigoma Serikali - Mkuu wa Mkoa Emmanuel Maganga Eneo - Mkoa 46,066 km² - Bara 37,037 km² - Maji 8,029 km² Idadi ya wakazi (2012) - 2,127,930 Jiografia Mkoa una eneo la km² 45,066 (sawa na 4.8% ya eneo lote la Tanzania) ikiwa km² 8,029 ndizo maji ya ndani (hasa Ziwa Tanganyika) na km² 37,037 ndizo nchi kavu. Takriban robo ya eneo la mkoa wa Kigoma hutumika kwa kilimo na ufugaji, karibu nusu ni misitu. Kwa ujumla eneo la mkoa ni tambarare ya juu inayoanza kwenye mita 800 juu ya UB karibu na Ziwa Tanganyika na kupanda hadi mita 1,750. Mito ya kudumu ndani ya mkoa wa K...

UK yawatahadharisha Watanzania Kuhusu Maandamano Ya Tarehe 26/04/2018

                London, Uingereza. Serikali ya Uingereza imewataka wananchi wake wanaoishi hapa nchini kuchukua tahadhari na maandamano ya kisiasa yanayotarajiwa kufanyika Aprili 26. Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo Aprili 24 imesema kwamba kuna raia zaidi ya 75,000 wanaoingia nchini hapa kila mwaka. Hivyo imewatahadharisha kujihusisha na maandamano hayo kwa madai kwamba wanaweza kupata madhara kutoka kwa jeshi la polisi. Katika taarifa hiyo ilitolewa tahadhari kwamba kwa sababu maandamano hayo yalishapigwa marufuku hivyo polisi ni lazima watatumia mabomu ya machozi au silaha za moto. “Hivyo muwe makini sana mnapokuwa kwenye mizunguko yenu muepuke mikusanyiko ya watu au watu wanaoandamana, muda wote muwe mnasikiliza vyombo vya habari, mjue nini kinachoendelea,’’ ilisema taarifa hiyo na kuongeza: “Ikiwa mnahitaji mawasiliano na namba ya dharura ya kupiga haraka ni 112 uliza huduma ya d...

Diamond Amtumia Salamu Ali Kiba Baada ya Kusikia Amefunga Ndoa

From Daimond "Ni Mwendo wa Picha za Suti tu sasa hivi, Maana nisije nikafungua hata kashati nikajikuta Centro...Pole yenu Wa zee wa Gym, Kama Muscat Round hii🤣🤣🤣.... Wadau Nimeambiwa King Kiba kaoa leo...Mfikishieni Salam zangu, za Ndoa njema, na Maisha yenye Furaha, Amani na Baraka tele...🔥🔥🔥 # SanaaImezaliwaUpya "