Skip to main content

Tundu Lissu Arejea d'salaam.



tundu lissu.

Lissu ambaye amekuwa hospitalini tangu Septemba 7, mwaka jana aliposhambuliwa nyumbani kwake Area D, mjini Dodoma, aliliambia shirika la utangazaji la BBC juzi, kuwa kwa sasa hana tena kidonda cha risasi na yupo tayari kurudi nyumbani.

"Sina tena kidonda cha risasi, nilipigwa mara 16," alidai Lissu (50) na kufafanua "sina tena kiungo kilichovunjwa".

"Nilikuwa nimevunjwa mguu mmoja mara tatu, mikono yote ilikuwa imevunjwa, nilikuwa na risasi nyingi mwilini, na vidonda vingi."

Lissu ambaye pia ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni, alisema viungo vyote vilivyokuwa vimevunjika vimeshaunga.

Alisema tangu aanze kupata matibabu amefanyiwa operesheni 17, nne zikiwa sehemu ya tumbo, lakini sasa hali yake ni nzuri.

Lissu alisema analazimika kurundi nchini kwa kuwa yeye ni Mbunge, Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Waziri kivuli wa Sheria na Katiba.

Alisema kwa majukumu hayo hawezi kwenda mafichoni.

"Siwezi kwenda mafichoni, siwezi kuikimbia nchi yangu, nitarudi Tanzania," alisema.

"Mimi ni mbunge, mimi ni kiongozi bungeni, ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, mimi ni msemaji wa sheria na katiba wa chama changu."

Hata hivyo, akizungumza na Nipashe jana kaka wa Lissu, wakili Alute Mughwai alisema familia bado haijapokea taarifa ya siku anayotarajia kurudi.

Alisema familia inachofahamu ni kuwa Lissu amefanyiwa operesheni ya 19 wiki chache zilizopita, hivyo kutakuwa na uangalizi wa afya yake.

“Hayo mahojiano aliyofanya juzi sijayaona, nitawasiliana naye leo jioni (jana) nimsikilize, lakini sisi kama familia hatujapata taarifa yoyote lini atarudi, wala hatuwezi kujua hadi tupewe taarifa na hospitali,” alisema wakili Mughwai.

Lissu alipoulizwa na BBC endapo amepata msaada wa matibabu kutoka serikalini, alisema chombo pekee chenye wajibu wa kumgharamia matibabu yake ni Bunge na "siyo serikali, wala Ikulu, wala mtu yoyote."

Aprili 19 Spika Job Ndugai alilieleza Bunge kuwa matibabu ya Lissu yanagharamiwa na Serikali ya Ujerumani.

Ndugai alisema amefahamu hilo kwa kupewa taarifa na Balozi wa Ujerumani nchini, Dk. Detlef Waechter, lakini pia akataja masharti matatu yanayopaswa kuzingatiwa, ili Bunge ligharamie matibabu yake hayo ughaibuni.

Matibabu ya mbunge huyo yalianzia kwenye Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Dodoma kabla ya kuhamishiwa katika Hospitali ya Nairobi, Kenya.

Chadema na familia yake wamekuwa wakilalama Bunge kukataa kugharamia matibabu ya mbunge huyo.

Hata hivyo, Spika Ndugai alieleza Bunge haliwezi kulipia gharama za matibabu za Lissu ughaibuni kwa kuwa hayakufuata taratibu za nchi ambazo wabunge na raia wa kawaida wanapaswa kuzifuata, ili serikali igharamiwe matibabu yao nje ya nchi.

Spika Ndugai alilazimika kutoa ufafanuzi huo bungeni kutokana na mwongozo ulioombwa kwake na Godbless Lema.

Mbunge wa Arusha Mjini Lema (Chadema), alitaka uongozi wa Bunge ueleze kwanini chombo hicho cha kutunga sheria hakitaki kugharamia matibabu ya Lissu.

Katika kujenga hoja yake, Lema alisema Lissu ana haki za kibunge na za raia wa kawaida kulipiwa gharama za matibabu na serikali, kama ilivyofanyika kwa Spika Ndugai ambaye ana siku chache tangu arejee nchini akitokea kwenye matibabu ya muda mrefu nchini India.

"Wakati Bunge la Bajeti likiendelea na vikao vyake, mbunge mwenzetu (Lissu) yupo Ubelgiji na Ofisi ya Spika bado inakataa kumlipia matibabu yake na haki zote za kimsingi anazo kama wewe (Spika),” Lema alisema na kueleza zaidi:

"(Spika) Ulipokuwa India kufanyiwa matibabu pamoja na ‘checkup’ (uchunguzi), serikali iligharamia matibabu yako. Mbunge bado yupo hospitali, lakini serikali haijaona wajibu.

“Kwanini serikali iligharamia matibabu ya Spika, lakini imeshindwa kuwajibika matibabu ya Lissu ambaye alishambuliwa kwa risasi Septemba mwaka jana hapa Dodoma?”

Akimjibu mbunge huyo, Spika Ndugai alisema mara nyingi amekuwa akijizuia kuzungumzia jambo hilo kwa sababu Lissu yupo hospitalini, lakini ameona ni vyema alijibu, ili kuondoa mkanganyiko.

Alisema kuna namna mbili ambazo matibabu ya wabunge na wananchi wanaweza kutibiwa ughaibuni kwa kufuata utaratibu wa umma.

"Utaratibu ni kwamba anayekwenda kutibiwa nje hususani wabunge, ili ‘cheque’ (hundi) iandikwe, ni lazima kuwapo barua yenye kibali cha (Hospitali ya Taifa) Muhimbili, kwamba mgonjwa huyu anahitaji rufani na nchi ipi apelekwe,” Spika Ndugai alisema.

Alisema zaidi: "Pili, awe na kibali cha Wizara ya Afya na kwa wabunge kutibiwa nje lazima Spika nipate barua ya kibali kutoka kwa Rais.

“Nikishapata hivi vitatu ndipo Mhasibu wa Bunge anaweza kuandika hundi kwa mbunge yeyote kwenda kutibiwa nje ya nchi.”

Kiongozi huyo wa Bunge alisema wakati Rais John Magufuli akifungua Bunge la 11 Novemba 20, 2015, alieleza namna asivyoridhishwa na wabunge wanavyosafiri ovyo kwenda nje ya nchi.

SAFARI ZA OVYO

Alisema Rais alisema katika miaka mitano ya uongozi wake, moja ya mambo atakayosimamia ni kuzuia safari za ovyo nje ya nchi.

"Huo ndiyo utaratibu. Mhasibu wa Bunge au Katibu wa Bunge hawawezi kutoa fedha yoyote kama havijakidhi vitu hivyo vitatu. Mbunge yeyote anayetibiwa nje, ni wengi waliotibiwa, wote kwa awamu hii wamekwenda kwa utaratibu huo,” alisema.

"Kwa hili sasa Spika anaandikaje hundi?

“Wakati utaratibu wake (kumwondoa Lissu nchini), Lema hukuwapo, wenzako walikuwapo walipompeleka Nairobi walijua na walioamua ni pande mbili tu; alikuwa mwakilishi wa familia pamoja na viongozi wako wa Kambi (Freeman Mbowe na Mch. Peter Msigwa) ambao wote ni wajumbe wa Tume ya Huduma za Bunge ambayo inashughulikia matibabu ya wabunge.”

Spika Ndugai alisema uamuzi wa kumpeleka Lissu Nairobi ulikuwa ni uamuzi wa rufani binafsi ambao gharama zake hazipaswi kuwa za serikali.

Alisema kwa utaratibu wa matibabu binafsi, wapo wabunge wengi ambao wamekuwa wakienda nje ya nchi, akiwatolea mfano wabunge wawili wa Chama Cha Mapinduzi (CCM); Charles Kitwanga (Misungwi) na Suleiman Nchambi (Kishapu).

"Kwa hiyo, ni kuchagua matibabu binafsi au ya umma. Ninyi (upinzani) mlichagua matibabu binafsi," Spika Ndugai alisema huku wabunge wa CCM wakimshangilia kwa kugonga meza.

Alisema hakuna mbunge yeyote anayebaguliwa na kama yupo, aeleze kama alifuata utaratibu huo na hakutibiwa kwa fedha za umma.

"Utaratibu ni utaratibu kwa watu wote. Kwa hiyo, tunashukuru hata hivyo, Wajerumani wanaomtibu Lissu kule Ubelgiji. Jambo hilo aliniambia Balozi wa Ujerumani,” alisema zaidi Spika Ndugai.

Comments

Popular posts from this blog

Niyonzima Apata Ajali Ya Gari

Haruna Niyonzima KIUNGO wa Simba, Haruna Niyonzima amenusurika katika ajali aliyoipata eneo la Mwenge jijini Dar es Salaam. Niyonzima amepata ajali hiyo juzi baada ya gari lake kupiga bonde na kupoteza mwelekeo wakati akirejea nyumbani kwake. Taarifa zinaeleza Niyonzima raia wa Rwanda alikuwa mwenyewe kwenye gari na akiwa njiani wakati anarejea nyumbani, akakutana na majanga hayo. Jana Championi  juhudi za kumpata Niyonzima aliyetua nchini kuichezea Yanga akitokea APR ya Rwanda na baada ya kumpata alithibitisha kupata ajali na kusema anamshukuru Mungu kwa kuwa haikuwa ajali kubwa. “Gari lilipoteza mwelekeo wakati nikiwa njiani narejea nyumbani na kuingia kwenye msingi. Bahati nzuri sikuwa katika mwendo mkubwa na kuna mtu alikatiza ghafla, nilipojaribu kumkwepa nikapoteza mwelekeo wakati najitahidi kurudi barabarani, nikapiga bonde gari likanishinda nikaingia msingini. “Haukuwa msingi mrefu, baadaye walikuja watu tukalitoa nikaondoka. Nashukuru sikuumia wala yule mtu sikumgonga

Rais Magufuli aitangaza Manispaa ya Dodoma kuwa Jiji

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, ameipandisha hadhi Manispaa ya Mji wa Dodoma na kuwa Jiji, huku akimtaja Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma wa sasa kuwa Mkurugenzi wa Jiji hilo jipya. Dkt. Magufuli amesema hayo leo Alhamisi, Aprili 26, 2018 wakati akihutubia wananchi waliojitokeza katika Viwanja vya Jamhuri, Dodoma wakati wa Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kutengeneza Tanzania. “Lengo la Serikali yetu kuhamia Dodoma lipo pale pale, hatuwezi kurudi nyuma. Sasa hivi zaidi ya watumishi 3,800 wameshahamia, mimi nitahamia Dodoma mwaka huu. Dodoma ndio Makao Makuu. Kwa mamlaka mliyonipa, natangaza rasmi kuanzia leo Aprili 26, 2018, Manispaa ya Dodoma itakuwa Jiji la Dodoma, mkurugenzi wake ataanza kuitwa Mkurugenzi wa Jiji”, amesema Dkt. Magufuli. Aidha, Rais Magufuli amesema maandalizi yote ya kisheria yaanze kutumika katika jiji hilo jipya nalitakuwa Jiji la kipekee kwa sababu lipo katikati ya Tanzania”.

Mama Kanumba Amjibu Wema Baada ya Kukataa Kuigiza Nae.

BAADA ya hivi karibuni staa wa filamu, Wema Sepetu kueleza maneno aliyoelezwa na aliyekuwa msanii wa filamu, marehemu Steven Kanumba enzi za uhai wake kwamba hataki kabisa mama yake mzazi, Flora Mtegoa aigize, mzazi huyo ameibuka na kufungukia ishu hiyo. Akipiga stori na Za Motomoto News, mama Kanumba alisema mwanaye huyo alisema hayo kwa sababu alikuwa akimtunza na kumlipa mshahara kama mfanyakazi lakini kwa sasa hayupo hivyo ndiyo maana ameingia kwenye sanaa ya uigizaji kwa kuwa bila hivyo angegeuka ombaomba jambo ambalo halipendezi. “Kanumba alisema hayo kwa kuwa alikuwa ananitunza yaani ananinunulia vyakula na kunilipa mshahara kila mwezi kama mfanyakazi lakini sasa hayupo, je Wema alitaka nishike bakuli nikaombe barabarani au? Maana kulima siwezi hivyo naona tu bora niigize ili niweze kujikimu kimaisha,” alisema mama Kanumba