Skip to main content

Wabunge waililia serikali kuhusu uhaba wa wauguzi na madaktari


Wabunge wameiomba serikali iliangalie kwa jicho la pekee tatizo la uhaba wa watumishi wa afya, hususani wauguzi na madaktari bingwa katika vituo, zahanati na hospitali na kulipatia ufumbuzi.

Pamoja na hayo, wabunge pia wamebainisha juu ya umuhimu wa serikali kuongeza jitihada za kutekeleza mpango wake wa kujenga zahanati katika kila kata kwa kuwa bado yapo maeneo ambayo hayana zahanati na kulazimika kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya. Wabunge waliyasema hayo bungeni Dodoma jana wakati wakichangia mjadala wa kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Bajeti ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ya mwaka 2018/19.

Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule (Chadema) alisema wilayani Kilosa hali ya upungufu wa watumishi ni kubwa kwani hadi sasa kuna mahitaji ya watumishi 1,025 na waliopo ni 474 tu sawa na asilimia 46. Alisema tatizo hilo limeongezewa uzito zaidi na utaratibu wa kupunguza watumishi wenye vyeti feki na hivyo kusababisha uhaba wa madaktari na wauguzi katika vituo vya afya, zahanati na hospitali ya Kilosa.

Naye Mbunge wa Kuteuliwa, Salma Kikwete (CCM) alisema afya ndio msingi wa maendeleo katika nchi yoyote endapo kuna ukosefu wa afya, uchumi wa eneo husika utapungua kwa kukosa nguvu kazi. Hata hivyo, alisema Mkoa wa Lindi mpaka sasa haujafahamu hatma yake ya kuwa na hospitali ya mkoa na wilaya, kwani hospitali iliyopo ya Sokoine imekuwa ikiitwa ya mkoa na wilaya na hivyo kuleta mkanganyiko.

“Pamoja na mkanganyiko huu bado mkoa huu una tatizo kubwa la uhaba wa wataalamu wa afya. Ni asilimia 28 pekee ya wataalamu wa afya ndio wapo Lindi na hivyo kuwa na upungufu wa asilimia 72 ya wataalamu hao,” alisisitiza Mama Kikwete. Mbunge wa Viti Maalumu, Amina Makilagi (CCM), alisisitiza juu ya umuhimu wa serikali kuliangalia tatizo la uhaba wa wataalamu wa afya kwa kuwa hospitali nyingi nchini zinakabiliwa na hali mbaya ya uhaba wa watumishi hao.

Kwa upande wake, Mariam Kisangi (Viti Maalumu - CCM), aliiomba serikali kuboresha hali ya matibabu katika Hospitali ya Mloganzila nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam kwa kuiongozea wataalamu zaidi wakiwemo madaktari bingwa na wauguzi kwa kuwa kwa sasa hospitali hiyo inazidiwa na wagonjwa.

Mbunge wa Vunjo (NCCRMageuzi), James Mbatia alisema ni wakati sasa wa serikali kuanza kushirikisha sekta binafsi na wawekezaji wakubwa wa ndani na nje ya nchi ili wawekeze katika sekta ya afya na kuongeza ubora wa huduma za afya nchini. “Tuwe wakweli japo wataalamu wetu wanafanya kazi kubwa, hatujawawezesha kibajeti ili waweze kufanya kazi yao. Serikali inabidi iweke mazingira rafiki na motisha kwa sekta binafsi wavutiwe ili wawekeze kwenye sekta hii...”

Comments

Popular posts from this blog

Historia ya mkoa wa kigoma

 Mkoa wa Kigoma  uko kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye postikodi namba 47000. Umepakana na Burundi na Mkoa wa Kagera upande wa Kaskazini, mikoa ya Shinyanga na Tabora upande wa mashariki na Mkoa wa Rukwa upande wa kusini. Magharibi umepakana na Ziwa Tanganyika penye mpaka na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Viwianishi: 4°53′S 29°40′E / 4.883°S 29.667°E Nchi Tanzania Wilaya 8 Mji mkuu Kigoma Serikali - Mkuu wa Mkoa Emmanuel Maganga Eneo - Mkoa 46,066 km² - Bara 37,037 km² - Maji 8,029 km² Idadi ya wakazi (2012) - 2,127,930 Jiografia Mkoa una eneo la km² 45,066 (sawa na 4.8% ya eneo lote la Tanzania) ikiwa km² 8,029 ndizo maji ya ndani (hasa Ziwa Tanganyika) na km² 37,037 ndizo nchi kavu. Takriban robo ya eneo la mkoa wa Kigoma hutumika kwa kilimo na ufugaji, karibu nusu ni misitu. Kwa ujumla eneo la mkoa ni tambarare ya juu inayoanza kwenye mita 800 juu ya UB karibu na Ziwa Tanganyika na kupanda hadi mita 1,750. Mito ya kudumu ndani ya mkoa wa K...

UK yawatahadharisha Watanzania Kuhusu Maandamano Ya Tarehe 26/04/2018

                London, Uingereza. Serikali ya Uingereza imewataka wananchi wake wanaoishi hapa nchini kuchukua tahadhari na maandamano ya kisiasa yanayotarajiwa kufanyika Aprili 26. Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo Aprili 24 imesema kwamba kuna raia zaidi ya 75,000 wanaoingia nchini hapa kila mwaka. Hivyo imewatahadharisha kujihusisha na maandamano hayo kwa madai kwamba wanaweza kupata madhara kutoka kwa jeshi la polisi. Katika taarifa hiyo ilitolewa tahadhari kwamba kwa sababu maandamano hayo yalishapigwa marufuku hivyo polisi ni lazima watatumia mabomu ya machozi au silaha za moto. “Hivyo muwe makini sana mnapokuwa kwenye mizunguko yenu muepuke mikusanyiko ya watu au watu wanaoandamana, muda wote muwe mnasikiliza vyombo vya habari, mjue nini kinachoendelea,’’ ilisema taarifa hiyo na kuongeza: “Ikiwa mnahitaji mawasiliano na namba ya dharura ya kupiga haraka ni 112 uliza huduma ya d...

Diamond Amtumia Salamu Ali Kiba Baada ya Kusikia Amefunga Ndoa

From Daimond "Ni Mwendo wa Picha za Suti tu sasa hivi, Maana nisije nikafungua hata kashati nikajikuta Centro...Pole yenu Wa zee wa Gym, Kama Muscat Round hii🤣🤣🤣.... Wadau Nimeambiwa King Kiba kaoa leo...Mfikishieni Salam zangu, za Ndoa njema, na Maisha yenye Furaha, Amani na Baraka tele...🔥🔥🔥 # SanaaImezaliwaUpya "