Skip to main content

Waziri Mkuu awataka Viongozi kuacha tabia ya kuingiza siasa kwa watu wanaoishi mabondeni

Serikali ya Tanzania kupitia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Wabunge na viongozi wengine kuacha tabia ya kuingiza siasa kwa watu wanaoishi mabondeni kwa kuwatetea kutohama maeneo hayo jambo ambalo linawapelekea kupata madhara pindi mvua kubwa zinaponyesha kama ilivyo sasa.

Waziri Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Aprili 19, 2018 Bungeni jijini Dodoma kwenye kikao cha 13 mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati akijibu swali la Mbunge Abdalla Mtolea ambapo alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kuhakikisha madhara yanayojitokeza katika jiji la Dar es Salaam na mvua kudhibitiwa? "kupitia Manispaa za jiji la Dar es Salaam na serikali yake kupitia wizara zake zinazo mipango ya kuboresha miundombinu katika miji yetu katika makao makuu ya mikoa na maeneo yote yale yanayokaliwa na watu wengi ikiwepo DSM.


Tunayo miradi sasa ambayo itaweza kuboresha miundombinu ikiwepo na bonde la Msimbazi ambalo linaleta madhara mengi... Mara kadhaa tumeshuhudia mvua hizi zinapoleta madhara kwa wale walioko mabondeni pamoja na serikali kuwaambia waondoke mabondeni tumekuwa tukiingilia sana utendaji kwa kuingiza siasa za kuwataka watu wabaki huku wengine wakijafanya wanawaonea huruma na kushindwa kutoka katika mabonde kutokana na utetezi unaotoka kwa watu wenye mapenzi yao binafsi", amesema Majaliwa. Waziri Mkuu ameendelea kwa kusema..

"Nitoe wito kama ambavyo tunaendelea kutoa wito na Waheshimiwa Wabunge kupitia Bunge hili tuwasii watanzania na kuwataka wote wanaoishi mabondeni wahame kwasababu mvua hizi zinapokuja wanapata madhara makubwa na hatimaye sasa hata katika kuwaokoa inakuwa shida. Kwa hiyo ni vizuri sasa tukashirikiana".

Pamoja na hayo, Majaliwa ameendelea kwa kusema "serikali kwa upande wake inaanda fedha kuhakikisha kwamba ile miundombinu ya mabonde ina boreshwa ili maji yaweze kupita kwa ulaini. Lakini watu waliokaa katika mabonde na yale maeneo yote waliyokataziwa waanze kuondoka mapema ili wasiweze kupata madhara pindi mvua nyingi zinapojitokeza".

Kwa upande mwingine, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewapa pole wananchi wote walioweza kupata maafa ya aina yeyote yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha nchini.

Comments

Popular posts from this blog

Historia ya mkoa wa kigoma

 Mkoa wa Kigoma  uko kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye postikodi namba 47000. Umepakana na Burundi na Mkoa wa Kagera upande wa Kaskazini, mikoa ya Shinyanga na Tabora upande wa mashariki na Mkoa wa Rukwa upande wa kusini. Magharibi umepakana na Ziwa Tanganyika penye mpaka na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Viwianishi: 4°53′S 29°40′E / 4.883°S 29.667°E Nchi Tanzania Wilaya 8 Mji mkuu Kigoma Serikali - Mkuu wa Mkoa Emmanuel Maganga Eneo - Mkoa 46,066 km² - Bara 37,037 km² - Maji 8,029 km² Idadi ya wakazi (2012) - 2,127,930 Jiografia Mkoa una eneo la km² 45,066 (sawa na 4.8% ya eneo lote la Tanzania) ikiwa km² 8,029 ndizo maji ya ndani (hasa Ziwa Tanganyika) na km² 37,037 ndizo nchi kavu. Takriban robo ya eneo la mkoa wa Kigoma hutumika kwa kilimo na ufugaji, karibu nusu ni misitu. Kwa ujumla eneo la mkoa ni tambarare ya juu inayoanza kwenye mita 800 juu ya UB karibu na Ziwa Tanganyika na kupanda hadi mita 1,750. Mito ya kudumu ndani ya mkoa wa K...

Stendi ya mabasi ya mikoani Ubungo kuhamishwa kupisha kituo cha mabasi ya Mwendo Kasi

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ipo kwenye majadiliano ya kuhamisha kituo cha Mabasi Yaendayo Haraka (UDART), kilichopo Jangwani na kukipeleka kwenye kituo cha Mabasi yaendayo Mikoani Ubungo (UBT). Hatua hiyo inatokana na eneo hilo la Jangwani kukumbwa na mafuriko ya mara kwa mara hali inayosababisha kuharibika kwa magari hayo. Akizungumza kwenye kikao cha kawaida cha madiwani jana, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita, alisema uamuzi huo umefikiwa ili kunusuru magari hayo yasiendelee kuharibika. Alisema Menejimenti ya Kampuni ya UDART na viongozi wa jiji wapo kwenye majadiliano kuhusu suala hilo ili waweze kufikia mwafaka. “Kwa sasa tupo kwenye majadiliano kwa ajili ya kuhamisha kituo cha mabasi yaendayo kasi(UDART) cha Jangwani tuweze kukipeleka Ubungo kwa sababu eneo la Jangwani limekuwa likikumbwa na mafuriko ya mara kwa mara mvua inaponyesha,” alisema Mwita. Alisema suala hilo linaendelea kufanyiwa kazi na Halmashauri ya Jiji hilo ipo kwenye mchakato wa kupanua Mt...

Mabasi ya Mwendokasi yasitisha huduma zake kwa muda

Kampuni inayotoa huduma katika mradi wa mabasi yaendayo haraka (UDART) imeamua kusitisha usafirishaji wa abiria kwa baadhi ya njia kuanzia saa 6:00 mchana kutokana na kufungwa kwa barabara ya Morogoro eneo la Jangwani kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha.  Hayo yameelezwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano UDART, Deus Bugaywa na kusema wamechukua maamuzi hayo kutokana na maji mengi ya mvua kupita juu ya daraja la Mto Msimbazi Jijini Dar es Salaam hali ambayo inahatarisha usalama wa abiria pamoja na vyombo vya usafirishaji.  "Kwa sasa huduma zinatolewa kwa njia za Mbezi - Kimara, Kimara - Morroco, Kimara - Magomeni Mapipa, Kivukoni - Muhimbili, Gerezani - Kvukoni, na Gerezani - Muhimbili. Huduma kamili zitarejea mara baada ya barabara kufunguliwa", amesema Bugaywa. Kwa upande mwingine, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano UDART, Deus Bugaywa amewaomba radhi wananchi wanaotumia usafiri huo kwa usumbufu ambao utajitokeza kwa namna moja ama ny...