Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza amesema wimbo wa Mwanaume Mashine haujafungiwa.
Ametoa kauli hiyo leo jioni Aprili 27, 2018 baada ya leo mchana Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu kuhoji sababu za kufungiwa kwa wimbo huo.
Shonza ametoa kauli hiyo wakati Bunge lilipokaa kama kamati kupitisha bajeti ya wizara hiyo mwaka 2018/19 baada ya Zungu kutaka kupewa jibu kuhusu ‘Mwanaume Mashine’ kutokana na maelezo ya Shonza na Waziri wa wizara hiyo, Dk Harrison Mwakyembe wakati wanajibu hoja za wabunge kuhusu bajeti hiyo kutoeleza sababu za kufungiwa kwa wimbo huo.
Mchana Zungu alihoji kufungiwa kwa wimbo huo wakati unamtaja mchezaji mahiri wa Simba.
Bunge limepitisha Bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo mwaka 2018/19
Comments
Post a Comment