Rapa anayefanya poa kwenye gemu la Muziki wa Hip Hop Bongo, Erick Msodoki ‘Young Killer’, amekuwa akiambiwa mara kadhaa na mashabiki wake abadilishe aina ya ‘kuchana’, ameibuka na kukataa kutekeleza hilo kwani ameona hakuna sababu ya kufanya hivyo.
Akizungumzia na Risasi Vibes, rapa huyo anayetamba na video ya Wimbo wa Shots, aliyom-shirikisha Khaligraph Jones kutoka Kenya, alisema kwamba hakuna maana kwani bado anaendelea na staili ileile ambayo inampatia hadi shoo zaidi ya tisa kwa mwezi.
“Sasa hapo nibadilike nini. Mtu unayepata shoo nyingi inaonesha wazi kwamba unakubalika. Siwezi kubadilika na nitaendelea kukimbiza zaidi na zaidi,” alisema Young Killer.
Comments
Post a Comment