tundu lissu. Lissu ambaye amekuwa hospitalini tangu Septemba 7, mwaka jana aliposhambuliwa nyumbani kwake Area D, mjini Dodoma, aliliambia shirika la utangazaji la BBC juzi, kuwa kwa sasa hana tena kidonda cha risasi na yupo tayari kurudi nyumbani. "Sina tena kidonda cha risasi, nilipigwa mara 16," alidai Lissu (50) na kufafanua "sina tena kiungo kilichovunjwa". "Nilikuwa nimevunjwa mguu mmoja mara tatu, mikono yote ilikuwa imevunjwa, nilikuwa na risasi nyingi mwilini, na vidonda vingi." Lissu ambaye pia ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni, alisema viungo vyote vilivyokuwa vimevunjika vimeshaunga. Alisema tangu aanze kupata matibabu amefanyiwa operesheni 17, nne zikiwa sehemu ya tumbo, lakini sasa hali yake ni nzuri. Lissu alisema analazimika kurundi nchini kwa kuwa yeye ni Mbunge, Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Waziri kivuli wa Sheria na Katiba. Alisema kwa majukumu hayo hawezi kwenda mafichoni. "Siwezi kwenda mafichoni, ...